Google PlusRSS FeedEmail

YALIOJIRI NJIANI KUELEKEA KIGOMA

Wadau  wa Habari wakiwa kazini ndani ya behewa kuelekea Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM

Treni ya iliyobeba wajumbe wa Sekretarieti na wananchi wengine ikielekea Kigoma.

Dk. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma maarufu ya wenyeji wa Saranda pamoja na Kepteni John Chiligati leo wakati ujumbe wa Sekretarieti unaoelekea Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahaman  Kinana, na  Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kepteni Mstaafu John Chiligati wakila mishikaki  baada ya kuwasalimu wana CCM  katika stesheni ya Saranda.

Shughuli za kila siku eneo la Stesheni ya  Saranda.

Dk.Asha Rose Migiro,Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakinawa mikono baada ya kupata mlo unaouzwa kando kando ya stesheni ya Saranda, viongozi hawa wamekuwa kivutio kabisa kwani kwenye ziara ya kuelekea Kigoma ,wamekuwa wakikutana na kila aina ya mwananchi .

This entry was posted in

Leave a Reply