Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM, UVCCM Bw. Martin Shigela akishiriki katika kupalilia shamba la Karanga katika kijiji cha Nkungwe Tarafa ya Mabembe Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembelea na kujionea shughuli mbalimbali na kukagua miradi inayotekelezwa na wananchi kwa pamoja na Serikali jana.
Sekretarieti ya CCM ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana iko mkoani Kigoma kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na sherehe za miaka 36 ya chama hicho zinazotarajiwa kufanyika Februari 3 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo, kulia ni Bi Fatma mmiliki wa na kushoto ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nkungwe wakati alipotembelea katika kijiji hicho jana