Google PlusRSS FeedEmail
Uwezo wa Mangula umesababisha  kiwewe kwa Chadema, Kilimwiko 
Na Charles Charles

 JUMATANO ya Novemba 12, 2012, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Kitila Mkumbo aliendeleza wimbi lake la kutokubaliana na kitu chochote kinachofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wala serikali yake.
Bofya hapa kwa habari zaidi.

UWEZO WA MANGULA WASABABISHA KIWEWE CHADEMA

Uwezo wa Mangula umesababisha  kiwewe kwa Chadema, Kilimwiko  Na Charles Charles  JUMATANO ya Novemba 12, 2012, Mjumbe wa Kamati Kuu na Msha... [Read More]

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha KANU Mhe Gideon Moi aliyemtembelea leo Novemba 29, 2012 katika hoteli ya Nairobi Serena jijini Nairobi

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA KANU GIDEON MOI JIJINI NAIROBI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha KANU Mhe Gideon Moi aliyemtembelea leo Novemba 29, 2012 katika hoteli ya... [Read More]

NA BASHIR NKOROMO
WALIOBOBEA katika medani ya falsafa husema, adui yako siyo lazima awe yule anayekunyooshea silaha ili kudhuru mwili au maisha yako, bali hata asiyekutakia mafanikio mema na kupuuza harakati zako za kimaendeleo ni adui tena namba moja.

Kwa mujibu wa wanafalsafa hao, tofauti na adui wa kukudhuru mwili au maisha yako ambaye akikushikia silaha unamtambua mara moja, asiyekutakia mema na kupuuza harakati zako za kimaendeleo, inakubidi uwe mweledi sana kumtambua haraka.

Wanasema, moja ya dalili za adui wa aina hiyo, ni yule ambaye ukifanya jambo linalokupeleka kwenye mafanikio makubwa analiponda kuwa halifai, na ukifanya baya linalokudidimiza anakusifia kwamba hilo ndilo zuri na la maana kuendelea nalo.

Ushauri unaotolewa na wanafalsafa hao, ni kwamba, ukishamtambua mtu kuwa ni adui yako, ukimsikia anakusifu kuwa jambo fulani unalofanya ni nzuri achana nalo mara moja, lakini akiliponda kwa nguvu zake zote kuwa unalofanya halina manufaa na kwamba ni la hovyo sana, basi jambo hilo ni jema, endelea kulifanya, yaani songa nalo mbele.

Katika gazeti moja la Raia Mwema, ambalo nimetokea kuliamini sana kuwa ni moja ya magazeti mahiri nchini na bila shaka nitaendelea kuamini hivyo, katika toleo lake la Novemba  28, mwaka huu, Mwandishi mmoja Evarist Chahali ambaye ameandika uchambuzi wake akiwa Uskochi, amejaribu kuandika uchambuzi alioupa kichwa cha  'Kosa la Kwanza kwa Kinana'.

Katika mtiririko wa uchambuzi huo ameeleza mengi akimsadifu Kinana hadi na wanasiasa za Marekani. Lakini  kwa kuwa sina muda na nafasi ya kutosha ya kukuchosha msomaji kwa kuyarejea aliyoandika, afadhali nijadili naye kuhusu jambo moja tu alilojaribu kulifanya jamii ilione kuwa ni kosa la kwanza alilofanya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, wakati wa mkutano wa CCM, uliofanyika mjini Geita wiki iliyopita.

Chahali anajaribu kushawishi wasomaji wakubaliane nake kwamba hatua ya Kinana kukabidhi leseni kwa wachimbaji madini wadogo 21, kwenye machimbo ya Mugusu, wakati wa mkutano huo eti ilikuwa ni aina ya kuhodhi mamlaka ya Wizara ya Nishati na Madini inayoratibu na kusimamia shughuli za madini nchini ikiwemo uchimbaji.

Tena anaenda mbali zaidi kwamba, kwa Kinana kufanya hivyo, inaweza kutafsirika kuwa ni mwendelezo wa vitendo vya kifisadi kwenye sekta ya madini hapa nchini, akisema kwamba huenda waliokabidhiwa leseni zile siyo wamiliki halisi wa leseni hizo, kwamba ni mamluki waliozipokea leseni hizo wakiwa ni vivuli vya watu wengine.

Pangine, hili la uwezekano wa kwamba waliopewa leseni walikuwa vivuli vya wengine, nisilisemee sana, kwa kuwa inawezekana. Lakini ili kulithibitisha hilo ni lazima anayetuhumu hivyo ajiridhishe kwa kujiuliza kwamba inawezekanaje hao wachimbaji wadogo 21, wawe mazuzu kiasi cha kushangilia kuzipokea leseni hizo wakati wanajua siyo zao, hasa ikizingatiwa kwamba hao ni miongoni mwa wakazi wa Geita ambao kilio chao cha kila siku ni kupata leseni za uchimbaji mdogo kwenye eneo hilo la Mgusu?

Na kama pengine walilipwa ili kuzipokea, mamia ya watu waliokuwa kwenye mkutano ule nao walishawishika vipi hadi nao wakashangilia hatua hiyo badala ya kuzomea? Maana waliokuwa kwenye mkutano huo wanawajua wote waliopakabidhiwa leseni hizo kwa sababu wote ni wakazi wa Geita.

Mimi ni miongoni mwa mamia ya watu waliokuwa kwenye mkutano huo  wa hadhara wa CCM ambao Kinana akikabidhi leseni hizo.

Ni kwamba, Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa imeshapitia taratibu zote za kutoa leseni hizo, na kilichofanyika pale ni tukio la kukabidhi leseni tu, kama vile Mkuu shule ya  Sekondari, Chuo cha Ufundi au Chuo Kikuu, ambavyo huandaa vyeti kwa ajili ya wahitimu kisha kazi ya kuwakabidhi wanaostahili ikafanywa na mgeni rasmi aliyealikwa kwenye mahafali.

Hivi Chahali na wengine wenye mtazamo kama yeye (kama wapo), kama mgeni rasmi akikabidhi hivyo vyeti kwa wahitimu waliostahili kwa kufuzu kwa vigezo, ndiyo inamaanisha kwamba amepora mamlaka ya shule au chuo husika?

Maana katika mkutano ule, ambao bila shaka asiye itakia mema CCM ulimkera, Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, kama Taasisi ya serikali inayotekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kilichopewa na wanachi ridhaa ya kuunda serikali, walikuwepo kutokana na kuitwa na mwajiri wao CCM ili kueleza wanavyosimamia kwa manufaa ya umma sekta ya madini.

Ili waweze kueleza vizuri mbele ya wananchi, ilikuwa ni lazima waje na ushahidi wa kutosha kuwaridhisha wananchi hao na mwajiri mwenyewe (CCM) juu ya usimamizi huo katika rasilimali hiyo adhimu Tanzania.

Chama Cha Mapinduzi ambacho ndicho chenye mkataba na wananchi tangu uchaguzi mkuu uliopita, kilikuwa tayari kina malalamiko kwamba wakazi wa Geita wanapata dhiki kutokana na kutopewa fursa ya kuruhusiwa kufanya uchimbaji mdogo katika mgodi wa Mugusu.

Sasa kwenye mkutano akaja Naibu Waziri wa Nishati na madini anayeshughulikia madini, Steven Masele. Alifika kuitika wito wa CCM yaani mwajiri wa serikali iliyopo madarakani, Kinana, kisha akapandishwa jukwaani  akahojiwa mbele ya wananchi, Je bwana mmefikia wapi katika kutatua kero hii ya wachimbaji wadogo? Masele akajibu " Tunazo leseni 21 kwa ajili ya wachimbaji wadogo waliofaulu vigezo ambazo tunaweza kuwakabidhi wakati wowote.

Kinana akamuuliza Masele " Je, leseni hizo zimepitia utaratibu wote vizuri na zipo tayari kuweza kukabidhiwa kwa hao wachimbaji? Masele akajibu, "ndiyo".

Baada ya hapo Naibu Waziri akamuomba Kinana kuwakabidhi leseni zao wahusika. Kinana akafanya kazi hiyo ikakamilika bila malalamiko, maana ilifuatiwa na nderemo na vifijo kwa waliopewa leseni hizo na pia kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Kimsingi mtiririko mzima wa kukabidhi hati hizo ulikuwa hivyo, lakini cha kushangaza ni kwamba mchambuzi wa makala hiyo, Chahali amejaribu, kutengeneza mawazo yananyowafanya baadhi ya wasomaji wake wadhanie leseni zile zilitolewa ghafla, papo hapo na CCM!

Bila shaka Chahali amebahatika kusoma na kuhitimu masomo yake, na bila shaka wakati wa mahafali alikabidhiwa cheti na mgeni rasmi, siyo Mkuu wa Chuo. Je, wakati anapokea cheti hicho alisita kwa kuhofia kwamba kwa mgeni rasmi kumkabidhi cheti hicho alikuwa anapora mamlaka ya mkuu wa chuo?

La msingi hapa ni kwamba,  hatua ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kuwakabidhi leseni wachimbaji hao wadogo halikuwa na ukiukwaji wowote na lilikuwa jema kwa CCM, ndiyo sababu kalamu za wasioitakia mema CCM wanaotamani wakiamka wakute imeondoka madarakani zimekemea tena kwa ukurasa mzima kwamba lilikuwa tukio baya na kosa la kwanza kwa katibu Mkuu huyo.

Kwa mtazamo wangu na kwa kuzingatia ushauri wa wanafalsafa, Kinana usiungame kwamba ulilofanya ni kosa la kwanza, isipokuwa ni moja ya matukio bora ya kwanza uliyofanya katika ziara yako ya kwanza tangu uteuliwe kuwa Katibu Mkuu wa CCM mapema mwezi huu kule mjini Dodoma.

Songa mbele, huku ukijitahidi kutojaribu kufanya hata moja ambalo hao wasioitakia mema CCM (ambao kwa dalili zao unawajua) watakusifu. Na siku ukiteleza ukalifanya jambo ukasikia wamekusifu hadharani, lichunguze kwa makini na uliache mara moja, usiendelee nalo.

HOJA MTAMBUKA:KINANA, KILA LINALOIJENGA CCM KWA WAPINZANI NI KOSA, SONGA MBELE

NA BASHIR NKOROMO WALIOBOBEA katika medani ya falsafa husema, adui yako siyo lazima awe yule anayekunyooshea silaha ili kudhuru mwili au mai... [Read More]

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA RAIS WA KENYA MWAI KIBAKI BAADA YA UFUNGUZI WA OFISI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, JIJINI ARUSHA JANA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Kenya, Mwai  Kibaki, ambaye ni Mwenyekiti... [Read More]

YANAYOJIRI KATIKA ULIMWENGU WA HABARI

Kushoto ni Makamo wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka akibadilishana mawazo na Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Dw, Mohamed Abdul-Rahman. [Read More]

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua  rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye  urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki  wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River
Viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki Jumatano Novemba 28, 2012 wamefungua rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga kwa upande wa Tanzania, na Namanga– Athi River kwa upande wa Kenya, kama sehemu ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi unaofanyika Nairobi, Kenya.
Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye  urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya shughuli za uzinduzi rasmi wa Makao Makuu Mapya za Jumuiya uliofanyika mapema siku hiyo hiyo jijini Arusha, kabla ya viongozi hao kuelekea Athi River kwa ufunguzi wa barabara hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Tanga–Horohoro, yenye urefu wa kilomita 66 pia nao umekamilika na  tayari imeanza kurahishisha usafiri na usafirishaji baina ya Tanzania na Kenya na nchi nyingine wanachama.
Barabara nyingine zilizopo katika mtandao wa barabara wa Jumuiya zinazoendelea kujengwa kwa upande wa Tanzania, ni pamoja na zile za mtandao wa Dar es Salaam-Isaka-Lusahunga na Mutukula hadi Masaka; Lusahunga-Nyakasanza hadi Rusumo, na Rusumo-Kigali hadi Gisenyi.
Nyingine ni Biharamulo - Mwanza - Musoma - Sirari - Lodwar – Lokichogio; Tunduma - Sumbawanga - Kigoma - Manyovu (Mugina) - Rumonge - Bujumbura - Ruhwa (Bugarama) – Karongi hadi Gisenyi, pamoja na ile ya Tunduma - Iringa – Dodoma - Arusha - Namanga hadi Moyale.
Ujenzi wa barabara hizi utarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na huduma baina ya nchi wanachama, na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji na vilevile gharama za kufanya biashara katika nchi za Jumuiya na hivyo kuvutia uwekezaji.

VIONGOZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA BARABARA YA ARUSHA-NAMANGA-ATHI RIVER

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua  rasmi... [Read More]

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (picha na Bashir Nkoromo)

 Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva, wakati wa mazishi hayo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Rais wa Bongo Movies Simon Mwakifyamba na Ofisa Habari wa Airtel Jackson Mbando, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashirb Nkoromo).
Mwili wa Marehemu ukiswaliwa kabla ya kwenda kuzikwa.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashir Nkoromo).
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole  Zaina Mkieli, Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashir Nkoromo).





NAPE AONGOZA MAELFU MAZISHI YA SHARO MILIONEA, MUHEZA‏

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa mu... [Read More]

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA OFISI YA CCM MAKAO MAKUU YA WILAYA YA BAGAMOYO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mjumbe wa NEC  Taifa, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi na wanachama w... [Read More]

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Sheikh wa Bagamoyo, Sheikh Abdallah Masoud Jembe, wakati alipofika nyumbani kwa sheikh huyo eneo la Ramiah mjini Bagamoyo, Nov 27, 2012 kwa ajili ya kumjulia hali kutokana na maradhi yanayomsumbua sheikh huyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi. Picha na OMR.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMJULIA HALI SHEIKH MKUU WA BAGAMOYO, ABDALLH MASOUD JEMBE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Sheikh wa Bagamoyo, Sheikh Abdallah Masoud Je... [Read More]

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM,  Nape Nnauye akitoa salam za Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es salaam. Maganga alifariki Jumamosi hii
 Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye shughyuli ya kuaga mwili wa msanii, John Maganga, Mwananyamala, Dar es salaam
 Msanii wa Bongo Movie,  Husna Maulidi 'Lishez', akituliwa na wenzake, Babby Candy na  Ketty wakati akilia kwa uchungu, wakati wa kuaga mwili wa Msanii wa Bongo Movie, marehemu  John Maganga
 Wasanii wa Bongo Movie wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Stephen Maganga, baba wa msanii John Maganga wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyama, Dar es salaam
Nape akizungumza jambo na Rais wa  Chama cha Filam za Bongo Movie

NAPE AIWAKILISHA CCM MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE, JOHN MAGANGA, DAR

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM,  Nape Nnauye akitoa salam za Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es sala... [Read More]

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI WA AJIRA KUPITIA MAFUNZO YA UFUNDI STADI, CHUO CHA UFUNDI VETA MKOA WA MTWARA

 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Elimu na Ufundi, Dkt.  Shukuru Kawambwa, (wa pili ... [Read More]

GEITA, TANZANIA
Baada ya Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na upotevu wa sh. milioni 16.6, za Halmashauri ya Kijiji cha Katoro mkoani Geita,  wakamatwe haraka na kufikishwa mahakamani, viongozi watatu wa kijiji hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Joel Mazemule (CHADEMA), wamekamatwa na walitarajiwa kufikishwa mahakamni leo kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.

Mwanri alitoa agizo hilo  wakati wa ziara  ya Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, iliyongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Abdulrahman Kinana, baada ya wananchi kuelezwa kuwa, viongozi hao wametafuna kiasi hicho cha fedha lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao.

Kamanda wa polisi Mkoani Geita, Leonard Paulo, katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jana, aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Mazemule (42) kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katoro, Fundi Makanza(44) na kuwa mwingine ni Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho kupitia CHADEMA, Charles Malegi (34).

Kamanda huyo alisema “Ni kweli tunawashikilia hawa viongozi watatu toka jana kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. Milioni 116.6 ambazo ni mali ya umma.”

Alieleza kwamba, polisi limefuatilia vielelezo vyote ikiwemo nakala halisi zilizotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Alexander Lumelezi na kujiridhisha, ndio maana wakawakamata.

Alisema, fedha hizo zinazodaiwa kutafunwa na watuhumiwa hao, zilitokana na ukusanyaji ushuru, toka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo mashamba, visima na maduka yaliyopo kijijini hapo.

Alifafanua kuwa, kati ya mwaka 2010/2011 kiasi kilichokusanywa na watuhumiwa hao kilikuwa sh. mil 21.3 lakini sh. Milioni  l6.6 zilipotea na hadi sasa hazijulikani zilipokwenda.

Kamanda Paul alisema, watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zinazowakabili.

VIONGOZI WA CHADEMA MBARONI KWA WIZI WA MILIONI 16 ZA UMMA GEITA

GEITA, TANZANIA Baada ya Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na upotevu wa sh. ... [Read More]

PICHA ZAIDI ZA ZIARA YA KATIBU MKUU ARUSHA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Sheikh Amr Abeid, baada ya kuvalishwa mavazi ya heshi... [Read More]

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA KINANA ARUSHA

 Kinana akisalimiana na Lowassa. Uwanja wa Ndege wa Arusha. Kushoto ni Ktb wa CCM Arusha, Mary Chatanda Pikipiki zikiongoza msafara wa Kinan... [Read More]

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika  mkutano wa hadhara unaofanyika jioni hii kwenye Uwanja  wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha (Picha na Bashir Nkoromo)

CCM YAFUNIKA ARUSHA, MAELFU WAFURIKA SHEIKH AMRI ABEID

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika  mkutano wa hadhara unaofanyika jioni hii kwenye Uwanja  wa Shei... [Read More]


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa mpira, mjini Geita mkoani Geita, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya mikoa minne kujitambulisha kwa wanachama na kukagua uhai wa chama ngazi za mashina na matawi na kusimamia na kueleza utekelezaji wa ilani ya Chama. (Picha na Bashir Nkoromo)

KINANA AKIHUTUBIA MAELFU YA WATU GEITA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa mpira, mjini Geita mkoani Geita, akiwa katika siku ya ... [Read More]

ZIARA YA KINANA GEITA‏

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu, Geita, katika mkutano wa hadhara uliofanyi... [Read More]


NA BASHIR NKOROMO, GEITA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Katoro Mazemule  na wenzake wanaodaiwa kuhusika na wizi wa sh. milioni 16.5 za Halmashauri ya kijiji hicho wafikishwe mahakamani haraka.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo, katika mji mdogo wa Katoro, mkoani Geita, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, ni lazima wahusika wote wa wizi wa fedha hizo wafikishwe mahakamani kwa kuwa ni jasho la wananchi.

Fedha hizo zinadaiwa kuliwa na Mwenyekiti huyo kwa tiketi ya Chadema, katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011 hali ambayo imezusha tafrani miongoni mwa wananchi na uongozi wa Halmashauri ya Kijiji hicho hadi sasa.

Nape alisema, ni lazima Mwenyekiti huyo na waliohusika wote wafikishwe mahakamani kwa kuwa kamati iliyoundwa kuchunguza upotevu wa fedha hizo ilishamaliza kazi yake na ripoti kukabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika.

"Kamati ya kuchunguza wizi wa fedha hizi ambazo ni mali ya wananchi ilishafanya kazi yake na kukabidhi ripoti kwa mamlaka zinazohusika, sasa kinachosubiriwa ni nini wahusika hawa kupelekwa mahakamani?", Nape alihoji na kuongeza;

"Sasa CCM kwa kuwa ndicho chama tawala, tunaagiza hatua za kuwapeleka mahakamani wahusika wote zichukuliwe haraka ili haki itendeke".

Nape alisema, kutotokea kwa wizi wa fedha hizo chini ya uongozi wa Halmashauri ya Kijiji hicho ambao upo chini ya chama hicho, ni dalili kwamba kujidai kwao kuwa wasafi na wapigania haki za wanyonge ni sawa na kilio cha mamba.

" Kila mara tumekuwa tukiwaambia acheni kuhadaiwa na Chadema, hawa siyo chama cha siasa ni kundi la wajanja fulani, sasa Wana Katoro mmejionea wenyewe, mmewajaribu mkawapa halmashauri yenu, fedha wamezitafuna sasa mnahangaika", alisema na kuongeza;

"Kwa kuwa mmepata funzo hili, bila shaka hamtaruidia tena, kwani mmeshafahamu kwamba kuikabidhi uongozi Chadema ni sawa na kumkabidhi fisi bucha".

Mapema, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma, alisema kwenye mkutano huo kwamba, kama hatua za kuwafikisha mahakamani wahusika hazitachukuliwa haraka, ataongoza wananchi wa Katoro kuandamana ili kuhakikisha hatua hizo zinachukuliwa.

Kabla ya mkutano huo, Nape alifungua shina la wajasiriamali la CCM, Bugayambele lenye wanachama  53 ambao hushughulika na kazi za kutengeza fenicha mbalimbali katika karakana yao iliyopo eneo hilo la Katoro.

Akifungua shina hilo, Nape aliahidi kuwapa sh. milioni moja kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao, ikiwa ni pamoja na kununua vitendea kazi kama randa za mbao, mashine ya kuchetrza mbao na ujenzi wa banda kwa ajili ya shughuli hizo.

NAPE: WALIOIBA FEDHA KATORO WAFIKISHWE MAHAKAMANI

NA BASHIR NKOROMO, GEITA CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Katoro Mazemule  na wenzake wanaodaiwa kuhu... [Read More]

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA KOREA, NCHINI TANZANIA.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo  na Balozi wa Korea nchini Tanzania... [Read More]

ZIARA YA KINANA SUMBAWANGA, AHUDHURIAA KIKAO CHA SHINA

Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Chipukuizi wa CCM, wakati wa mapokezi yake kwenye Uwanja wa Ndege w... [Read More]