Google PlusRSS FeedEmail

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA KOREA, NCHINI TANZANIA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea nchini Tanzania, IL Chung, wakati alipofika ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Nov, 23, 2012

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Korea nchini Tanzania, IL Chung

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal,leo amekutana na Balozi wa Korea hapa nchini Bw. IL Chung ambae alimtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam ambapo wamefanya mazungumzo juu ya mahusiano yaliyopo baina ya Tanzania na Korea na kusisitiza kuwa mahusiano hayo ni vizuri yakiboreshwa na kuthaminiwa ile kuendeleza urafiki uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Pia, Makamu wa Rais amezungumza na mgeni wake huyo juu ya kuangalia uwezekano wa Korea kuisaidia Tanzania katika suala zima la utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati zenye madhara chanya kwa mazingira, Mheshimiwa Makamu wa Rais alieleza kuwa hivi sasa Tanzania ina tatizo kubwa la mazingira kutokana na uharibifu mkubwa unaotokana na matumizi ya miti kama nishati muhimu kwa wananchi hasa wa vijijini.

This entry was posted in

Leave a Reply