DAR ES SALAAM, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya mnazi mmoja, ambapo yamefanyika mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Sekretarieti Mpya iliyoundwa baada ya Mkutano Mkuu wa Chama uliofanyika hivi karibuni katika Mji wa Dodoma.
Mkutano huo mahsusi kwa mkoa wa Dar es Salaam kufanya sherehe za mapokezi ya viongozi wapya waliochaguliwa na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kuwa safu mpya ya kukisimamia, kukiimarisha na kukiendeleza Chama..
Mkutano huo ambao ulianza majira ya mchana wa saa nane na kumalizika saa kumi na mbili ulitawaliwa na matukio mbalimbali zikiwemo hotuba muhimu kutoka kwa viongozi hao wapya ambao walisisitiza kuwa sasa kikosi kamili kimetimia na yale ambayo yalikuwa yanawakwaza wanaCCM likiwemo suala la Rushwa katika chaguzi, upendeleo na kupanga safu ya uongozi kwa maslahi binafsi, Katibu Mkuu wa Chama Hicho alisisitiza juu ya Kuondoa kabisa tatizo la UBINAFSI ambalo ndio chanzo kikubwa cha makundi na migogoro katika chama hicho.
*ZIAFUATAZO NI PICHA ZA BAADHI YA MATUKIO YALIYOSISIMUA
Mmoja wa wanan-CCM waliohudhuria sherehe hizo, akiwa na bango kufikisha ujumbe wa wengi
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa wimbo maalum wa CCM wakati wa sherehe hizo
Asley na Tundaman wakitoa burudani kwenye mkutano huo
Mapema Rais Kikwete alikabidhiwa shada la maua na mtoto maalu
Mama Salma Kikwete ambaye pia alikuwepo mstari wa mbele katika sherehe hizo, alikabidhiwa shada la maua