Kutokana na kwamba lengo la CCM kufungua Blogu hii ni kuwezesha wana-CCM na wadau wote ndani na nje ya Tanzania kupata taarifa mbalimbali za Chama na za kijamii, huku wao pia wakipewa fursa ya kutoa maoni kupitia blogu hii, Msomaji wetu mmoja, Dk. Thabiti Leonard NyuyabaliweMimi ni Dr,Thabiti Leonard .F.Ntuyabaliwe (Pichani), wa jijini Dar es Salaam, ametutumia maoni yake yaliyotanguliwa na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete kwa kuchaguliwa tena kushika wadhifa huo. Kutokana na kuthamni mchango wa wadau wetu kupitia blogu hii, Maoni na pongezi hizo tunatoa kama alivyoyaandika.
Pia nachukuwa na Fasi hii kushukuru wajumbe wa Mkutano mkuu CCM Taifa kwa mchango mzuri waliyoutowa kwa kuimalisha Chama Tawala CCM, na pia kwa Kuchagua viongozi mahili wa kukitumikia chama kwa muda wa Miaka Mitano Ijayo.
Nampongeza Pia Mh.Dr JK kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kipindi cha miaka mitano Ijayo,Pia na wapongeza Makamu Mwenyekiti ZNZ,na Makamu Mwenyekiti Bara,walichaguliwa kwa kishindo,Mwenyezi Mungu Awe na nyi na awaongoze katika Uongozi wenu,wa kukitumikia chama na Taifa kwa Ujumla.
Hongera Pia Mh.Dr,Jakaya M.Kikwete, kwa safu ya sekretarieti uliyoweka,ni watendaji Hodari,tunategemea Chama sasa kuwa na ushindi wa kishindo katika kurejesha mitaa,kata,na majimbo tuliyopoteza kwa uzembe wawazi wa sisi wanaCCM wenyewe.
Ushauri,wangu, kwa viongozi Tembeeni huku mukishuka chini kabisa ngazi za Matawi na Kata,Kutoa Semina Elekezi hasa kwa Viongozi wa Matawi na Kata, maana hawa ndiyo waliyo karibu na wapigakura wetu, ambao ni wananchi,niwazi kabisa uwezo wa viongozi wao kuwa mudogo,wanashindwa kujuwa kiwango cha matatizo ya wanachama waliyo wachagua.ikumbukwe kuwa huwa wanapojinadi kugombea nafasi hizo walizonazo, waliahidi kufanya mambo kadha wakadha, na walikuwa nania njema kabisa ya kuyatekeleza matakwa ya wapiga kura wetu, lakini, inafikia hatuwa wanakuwa njia panda,.uwezo wakubuni mbinu za kutatua matazo hayo unakuwa mudo mno.
Pia hali ya maisha ya badhi ya viongozi wetu wa Matawi na Kata, hasa watendaji yanasababisha washindwe kutekeleza jukumu lao la utumishi ndani ya Chama.pia kutokana na hali hiyo uwaminifu wao kwa wanachama na wananchi kwa ujumla unapungua.
Kutokana na hayo na mengine mengi ambayo, siwezi kuyaeleza katika ujumbe huu,.ni vyema kukawekwa mikakati ya kubuni miradi ya muda mufupi na muda mrefu, ili kusudi watendaji wa chama Matawi na Kata,waweze kuwezeshwa, lakini pia hata wajumbe wa nyumba kumi wawezeshwe japo kununuliwa karamu na karatasi. niko tayali kujitolea kutoa semina elekezi ikiwezekana hata taifa zima kwa ajiri ya CCM.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI CCM.