DAR ES SALAAM, TANZANIA
Gazeti la Mwananchi la leo katika habari yake iliyoongoza katika ukurasa wa kwanza, limeandika kwamba, Sekretarieti Mpya ya CCM imepondwa kila kona, huku mmoja watu mashuhuri waliohusishwa kuponda Sekretarieti hiyo akiwa ni Askofu Method Kilaini. Kufuatia habari hiyo, Kilaini amekanusha habari hiyo. Nasi tunaichapisha hapa kama tulivyoipata.
Kwa masikitiko makubwa nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya uongozi na sekretariati ya CCM. Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na wala sina nia au sababu ya kuuponda uongozi huo. Ni vibaya kwa gazeti lo lote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. Kama ni waugwana natumaini watasahihisha waliyoyaandika. Nasikitika sana kwa walikwazwa na hilo. Askofu Kilaini
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese