Google PlusRSS FeedEmail

KINANA ATUA TABORA, AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia viongozi wa mkoa wa Tabora alipotua kwa muda mkoani humo akiwa akitoka Rukwa kwenda Geita asubuhi hii

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akipotua kwa muda mkoani humo akiwa akitoka Rukwa kwenda Geita asubuhi hii


Na; Bashir Mkoromo, Tabora

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amefanya ziara ya kushtukiza katika Mkoa wa Tabora asubuhi hii ambapo amekutana na Mkuu wa Mkoa huo Bi Fatma Mwasa na pia kukutana na viongozi wa Chama wa Mkoa ambapo alifanya kikao kidogo na viongozi hao akisisitiza juu ya utekelezaji wa Ilani na maagizo ya Mkutano Mkuu wa kufanya Mikutano ya ndani na nje na kutembelea mashina. Alisisitiza kuwa litakuwa ni jambo la ajabu ikiwa yeye kama Katibu Mkuu wa Chama katika ziara zake anatembelea na kufungua mashina kisha viongozi wa Mkoa ama eneo husika hawatembelei mashina hayo wala kufuatilia maendeleo yake.

Ndugu Kinana alitua Tabora Asubuhi hii akiwa njiani kutoka katika Mkoa wa Rukwa ambako alifanya Mkutano wa Hadhara na pia kufungua shina la Isesa wilayani Sumbawanga. Ndugu Kinana hivi punde ataendelea na Ziara yake, ambapo ataelekea Geita ambako atafanya Mkutano wa Hadhara na pia kufuatilia kero za wachimbaji wadogo pamoja na hali za waajiriwa katika migodi.

This entry was posted in

Leave a Reply