Google PlusRSS FeedEmail
Nape Nnauye-Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi
-->Yadai orodha yake inalenga kupotosha  tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.
--> Inataka kuwaokoa wabunge wa Chadema katika sakata hilo.
--> Yasema suala la tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe kuwa la kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.

Akizungumza na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.

"Mfano mzuri wa juhudi hizi ni kitendo cha Tundu Lissu, ambaye ni  mbunge wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kkambi ya upinzani Bungeni cha kutoa aliyoiita orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara na TANESCO na kwamba ndio watuhumiwa wa rushwa inayozungumziwa", Alisema Nape na kuongeza;

"Cha kushangaza orodha yake ilikuwa na wabunge wa CCM peke yake wakati wote tunajua kuwa yapo majina ya baadhi ya wabunge wa vyama vingine hasa Chadema, yanayotajwa katika orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hii".

Nape alisema juhudi hizo za Lissu na wenzake zinalengo la kuuficha ukweli na kujaribu kuwalinda watuhumiwa wa uhalifu wanaotokana na Chadema.

"Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.

Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.

"Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.

Nape alisema  CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri na umahiri wao mkubwa waliouonyesha kwa muda mfupi waliokaa kwenye wizara hiyo.

"Tunaamini uzalendo walioonyesha katika kusimamia wizara hii,utaigwa na watumishi wengine wa umma katika kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali za nchi zinalindwa ili kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanatimia. Tunaunga mkono jitihada zao", alisema Nape.

Alisema, pia CCM inalipongeza bunge kwa kuendelea kusimamia serikali na rasilimali za nchi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa ya maendeleo.

"Tunawaomba waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.

CCM yaishukia CHADEMA suala la TUHUMA za Rushwa kwa wabunge.

Nape Nnauye-Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi -->Yadai orodha yake inalenga kupotosha  tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge. --... [Read More]


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amewataka
wahitimu na wale wote wenye kutafuta fursa za ajira Serikalini kujijengea utamaduni wa kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira mara kwa mara kwani kila nafasi za ajira zinapojitokeza huwekwa katika tovuti hiyo ili kutoa fursa kwa wadau walioko nje na ndani ya nchi kuweza kuziona kwa urahisi.

Amesema hayo leo, wakati akiongea na mwandishi wa habari ofisini kwake aliyetaka kujua fursa za ajira zilizoko na taratibu za mchakato wa ajira tangu kutolewa kwa tangazo hadi kupangiwa kituo cha kazi.

Daudi amesema, kwa mfano mwananchi yeyote akitembelea katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira hivi sasa ataona tangazo la kuitwa kazini kwa waombaji kazi waliofaulu katika usaili uliofanyika mwezi Juni, 2012 ambao wanatakiwa kuripoti kwa Waajiri; Wakala wa Vipimo, pamoja na kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii. 

Mbali na hilo, pia watakuta tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa wale waliokidhi vigezo kulingana na nafasi walizokuwa wameomba kama zilivyokuwa zimetangazwa kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Chuo cha Mipango Dodoma, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na taasisi nyinginezo.

Aliongeza kuwa katika Tovuti hiyo watakuta pia tangazo la nafasi za kazi 194 zikiwemo nafasi za Wakurugenzi, Wakufunzi Waandamizi wa Vyuo, Wakufunzi Wasaidizi, Wahandisi, Mafundi Sanifu, Wakaguzi wa ndani wa hesabu, Makatibu Mahsusi, Walinzi, Wapishi na kada nyinginezo.
Aidha, amesisitiza ni muhimu kwa waombaji kuzingatia masharti ya tangazo pindi wanapotuma maombi yao kwa njia ya posta ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata fursa ya ajira serikalini maana mchakato wa ajira hufuata Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira alimaliza mahojiano yake kwa kuitaja tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuwa ni www.ajira.go.tz kwa wale wasioifahamu ili waweze kuifahamu.

WANANCHI WAMEHIMIZWA KUTEMBELEA TOVUTI YA SEKRETARIETI YA AJIRA

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amewataka wahitimu na wale wote wenye kutafuta fursa za ajira... [Read More]

UJUMBE WA WANAFUNZI

[Read More]

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bibi Antonia Mbagalla (85) katika kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki leo (Jumapili). (Picha na Freddy Maro)

RAIS KIKWETE ASALIMIANA NA BIBI WA MIAKA 85 KIJIJI MSOGA LEO

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bibi Antonia Mbagalla (85) katika kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakat... [Read More]

Kilimanjaro mountain burger ni moja ya burger zinazopatikana katika mgahawa wa New African pale Monrovian Center ,mjini Sumbawanga.

BURGER YA KILIMANJARO NDANI YA SUMBAWANGA

Kilimanjaro mountain burger ni moja ya burger zinazopatikana katika mgahawa wa New African pale Monrovian Center ,mjini Sumbawanga. [Read More]

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi  hanga la Precision Air lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Precision Air Bwana Michael Shirima.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi hanga la Precisionair katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere leo asubuhi.Kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Precision air Bwana Michael Shirima.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya ndege za shirika la ndege la Precision ikifanyiwa matengenezo katika hanga jipya la shirika hilo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hanga la shirika hilo la ndege lililojengwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu  Julius Nyerere(picha na Freddy Maro).Habari hii inapatikana pia TANZANIA VISION BLOG

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINMGI UJENZI HANGA LA PRECISION AIR DAR

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi  hanga la Precision Air lililopo katika u... [Read More]


Kampteni Komba akiwa na mkewe, Salome Komba
 nyumbani kwake Kawe leo
Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni mstaafu, John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa upasuaji kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu wake wa kulia.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo, Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi, Kawe,  Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini,  Juzi,  baada ya kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad nchini India tangu mwanzoni mwa wezi huu.

Alisema, aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu wa Bunge John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu hapa nchini kwa sababu ya mgomo wa madaktari.

"Siku napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya kwanza ya mgomo wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge na kisha nikamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa mamlaka yake akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda kutibiwa nje", alisema Komba.

Alisema, uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande wa mguu wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo 138 wakati wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa mwili wake ni kilo 90 au 100 tu.

"Amesema, baada ya matibabu amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 128 ambao hata hivyo ametakiwa kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi ambazo atalazimika kupumzika nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi Septemba mwaka huu kama alivyoelekezwa na madaktari.

Akizungumzia upasuaji ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa tano na kukamilika bila matatizo katika upasuaji huo ambao alisema sehemu iliyopasuliwa ni ya ukumbwa wa futi moja.

Alisema, hata hivyo baada ya upasuaji huo, hakuweza kurejea katika wodi ya kawaida, kwa sababu majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali, presha, hivyo akalazimika kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) kwa siku tano.

"Sasa nimerejea nikiwa mzima, kwa sasa natumia fimbo hii, ili kuwezesha uzito uzilemee upande wa kulia nilikopanyiwa upasuaji, lakini sijambo kabisa", alisema Komba.

Komba alilaani baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwamba katika kuugua kwake alikuwa mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.

"Jamani ninyi waandishi wa habari, jizoesheni kuandika habari zilizokamilika siyo kurashia-rashia tu na kuzusha uongo, mfano gazeti moja liliandika eti naugua figo nipo mahututi, wakati si kweli kabisa, ilikuwa jambo rahisi tu, kuja hapa nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke wangu lingepata kwa uhakika ninachoumwa", alisema Komba.

JOHN KOMBA AREJEA BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI INDIAj

Kampteni Komba akiwa na mkewe, Salome Komba  nyumbani kwake Kawe leo Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge ... [Read More]

SIKU YA MASHUJAA ILIVYOFANA

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Juli 25, 2012 ameongoza Watanzania katika kuadhimisha siku ya Mashujaa Kitaifa katika Bust... [Read More]

 Diwani wa Kata ya Kwadelo,Kondoa mkoa wa Dodoma,  Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto) akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani (kushoto), Gabriel Galahenga, baada ya kuwakabidhi wakulima hao matrekta maane, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja  ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa  zilizobaki katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo.
 Diwani Kariati akikabidhi funguo ya trekta kwa mmoja wa wakulima  wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani. Wengine ni wakulima wa Kata hiyo, Alifa Hulufya (kulia), Chundu Damiani (wapili kushoto) na Gabriel Halahenga (watatu kushoto) na kati yao ni Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan.
 Diwani Kariati akikabidhiwa barua na mkulima wa Kwadelo,  Gabriel Halahenga, wakati wa hafla ya diwani huyo kukabidhi matrekta maane kwa wakulima wa kijiji hicho leo, Ofisi za Suma KJT, Mwenge, Dar es Salaam.  Wengine ni,  Alifa Hulufya (kulia), Chundu Damiani (wapili kushoto) na Gabriel Halahenga (watatu kushoto) na kati yao ni Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan. Barua hiyo ni kwa ajili ya Dhukurani kwa Mkuu wa JKT kutokana na Suma JKT kukubali kuwapa matrekta wakulima wa Kwadelo, kwa malipo ya nusu ya gharama na kumalizia deni katika kipindi cha miaka minne baadaye.
 Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan akifurahia jambo na Diwani Kariati wakati wa makabidhiano ya trekta hizo.
 Diwani Kariati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi trekta nne kwa wakulima wa kata yake leo. Habari hii inapatikana pia kwenye Blogu yetu ya Tanzania Vision Blog...BONYEZA HAPA UONE

KATA YA KWADELO, KONDOA WAZIDISHA UTEKELEZAJI KILIMO KWANZA

 Diwani wa Kata ya Kwadelo,Kondoa mkoa wa Dodoma,  Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto) akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abda... [Read More]

KUKABIDHI NYARAKA ZA KIUTENDAJI, TAWI LA CCM MOSCOW

Yah: KUKABIDHI NYARAKA  ZA KIUTENDAJI, TAWI LA CCM MOSCOW- 24 July 2012 BOFYA HAPA KWA TAARIFA KAMILI [Read More]

MTAA WA MKUNGUNI

Mtaa wa Mkunguni umebadilika kwa kasi sana,na haya ndio mabadiliko yanayodhihirisha kukua kwa mji na maendeleo kwa jumla. Mtaa wa Mkunguni j... [Read More]

Rais John Atta Mills wa Ghana amefariki dunia siku ya Jumanne baada ya kuugua usiku wake siku ya Jumatatu.
  Rais John Atta Mills alibakisha miezi michache asimame tena kutetea nafasi yake katika uchaguzi mkuu wa rais nchini humo.
Ikumbukwe Ghana ndio nchi ya pili kuzalisha zao la cocoa kwa wingi duniani na Mills alikuwa na mkakati wa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchini Ghana.

RAIS WA GHANA AFARIKI DUNIA

Rais John Atta Mills wa Ghana amefariki dunia siku ya Jumanne baada ya kuugua usiku wake siku ya Jumatatu.   Rais John Atta Mills alibakisha... [Read More]

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI MBEYA

 Rais Dkt.Jakaya   Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo katika Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(wapili kushoto), balozi wa jumuiya ya ulaya ... [Read More]

MKUTANO WA CCM KIGOMA MJINI

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tzeba akihutubia kwenye  mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye  Uwanja wa Community ... [Read More]

NAPE,MAWAZIRI WATUA KIGOMA, KUUNGURUMA UWANJA WA COMMUNITY CETRE MWANGA MCHANA HUU‏

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na ujumbe wake wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kipamba mkoani Kigoma. Kushoto mwisho ni Waziri S... [Read More]

MAANDALIZI MKUTANO WA CCM KIGOMA YAIVA‏

Bendera za CCM  zilizopambwa kwenye Uwanja wa Community Cetre, Mwanga, mkoani Kigoma, zikiwa zimeunakishi uwanja huo, leo jioni ikiwa ni s... [Read More]

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kesho, Jumapili, Julai 22, kinatarajiwa kuutikisa mkoa wa Kigoma, kwa mkutano wake mkubwa wa hadhara, utakaofanyika kwenye Viwanja vya Communicy Cetre mjini Mwanga mkoani hapa.

    Mkutano huo mkubwa umepangwa kuhutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, na baadhi ya mawaziri walioalikwa kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika sekta wanazohusika nazo.

    Mkutano huo, umepangwa kuanza mapema kwa kuwa unatakiwa kumalizika saa kumi jioni ili kuwapa fursa wananchi waliofunga kwenda kufuturu baada ya kushinda ana swaumu ya Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

   Awali Mkutano huo ulikuwa ufanyike, Ijumaa iliyopita, lakini ukalazimika kusogezwa mbele baada ya taifa kuingia katika maombolezo ya siku tatu, kufuatia ajali ya meli iliyotokea Zanzibar ambapo watuzaidi ya 50 wamefariki dunia.

  Katika mkutano huo wa kesho Jumapili, Nape na baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri walioalikwa akiwemo Steven Wasira na Aggrey Manri,  wanatarajiwa kueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Kigoma na Tanzania kwa jumla.

  Pia wanatarajiwa kueleza sera za CCM, na kueleza wananchi wa Kigoma, nini CCM imefanya, inafanya sasa na inatarajiwa kufanya nini baadaye katika kukifanya chama hicho na serikali yake, kuendelea kuwa makini na imara katika kuliongoza taifa la Tanzania. 
 Kufuatia mkutano huo kuahihirishwa  karibu kona zote za mji wa Kigoma na vitongoji vyake kama Ujiji, Kahabwa, Gungu na Mwandiga, wamekuwa wakijadili kuhusu mkutano huo, kwenye vijiwe vya kahawa, vituo vyua daladala na kwenye mikusanyiko hasa ya vijana, hamu kubwa ikiwa ni kutaka kumsikiliza Nape na wabunge watakaopanda jukwaani kwa mtindo wa aina yake.
  Pia baadhi ya watu wameonyesha hamu ya kuhudhuria mkutano huo kutokana na staili ambayo inaelezwa kuwa ni mpya na nzuri ya CCM kuwapeleka kwenye mikutano ya hadhara baadhi ya mawaziri kueleza wanavyosimamia utekelezaji wa ilani ya Chama kwenye sekta zao.
 "Kwanza mimi ningependa nimsikie Nape, nasikia ni msema kweli kama kuna jambo huwa hasiti kusema hata kujwaani, na pia nitapenda niwasikie mawaziri watakaowaleta kwa sababu kwa muda mrefu hatujawahi kumsikia hapa Kigoma waziri yeyote akisimama jukwaani kwenye mkutano wa hadhara kueleza utekelezaji wa ilani", alisema Joseph Chishako wa Mwandiga.

NAPE , MAWAZIRI KUHUTUBIA KESHO KIGOMA‏

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kesho, Jumapili, Julai 22, kinatarajiwa kuutikisa mkoa wa Kigoma, kwa mkutano wake mkubwa wa hadhara, utakaofany... [Read More]

Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi imemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia Vifo vya Watanzania waliofariki katika ajali ya boti ya Skagit iliyotokea hivi karibuni maeneo ya chumbe kisiwani Unguja.

Salamu hizo zimefikishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Chonjo, ambae alisema kuwa wananchi wake wamemuomba afikishe salamu za rambirambi kwa Mheshimiwa Rais, na ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata majeruhi.

Bi Chonjo alisema kuwa huu ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao ni majonzi yetu, Watanzania wote. Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa.

Aidha  amewapongeza maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa meli binafsi, kwa juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa na maafa haya makubwa na ya aina
yake. Ambapo alisisitiza na kuomba  waendeleze juhudi hizo kwa manufaa ya Nchi yetu.

  ’’Hakika Inauma sana kuona Watanzania wakipoteza maisha  hasa tukikumbuka vifo vingi vya MV Spice Islander miezi 10 iliyopita Wananchi wangu wameniomba nikuombe uunde tume ya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na njia ya kunusuru vifo vya Majini vinavyopoteza nguvu kazi nyingi kwa Maendeleo_Alisema DC. Chonjo" Kutokana na ajali hiyo na msiba huu mkubwa,Tumeungana nawe Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,katika maombolezo ya taifa ya siku tatu.

WILAYA YA NACHINGWEA YAGUSWA NA VIFO VYA WATANZANIA AJALI YA BOTI KISIWANI UNGUJA

Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi imemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikw... [Read More]


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe(kulia) akiwa katika eneo la msitu wa Hifadhi ya Katavi, eneo maarufu kwa jina la lyamba lya mfipa.
 
 
Na Kibada Kibada-Katavi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe ameagiza kampuni ya utafiti na uchimbani madini ya Red O-Mining ltd kutoka China  kusimamisha mara moja shughuli zote za utafiti kwa kuwa wamekiuka sheria za nchi kwa kufanya utafiti ndani ya  pori la hifadhi ya wanyama   la Rukwa Lukwati lililoko Hifadhi ya Taifa ya  Katavi  kinyume na sheria.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wawekezaji hao wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa Madini katika pori hilo la hifadhi kinyume na taratibu za kisheria za nchi pamoja na kuwa wanayo leseni  ya kufanya utafiti inayowaruhusu waliyoipata kutoka wizara ya nishati na Madini lakini hawana kibali kinachowaruhusu kufanya utafiti ndani ya hifadhi.
Pamoja na kupata leseni hiyo walipatiwa barua  kutoka wizara ya Maliasili na Utalii na idara ya  mazingira inayowaelekeza kuwa wakifika eneo la kufanyia utafiti wawaone wamiliki wa eneo kupitia ofisi za wanyama pori wilaya husika,ya Mpanda lakini hawakufanya hivyo, badala yake waliamua kuingia katika pori hilo la hifadhi la Katavi na kuendelea na shughuli zao za kiutafiti bila kuwa na kibari cha kufanya shughuli hizo ndani ya hifadhi kwa kuwa ni kinyume na taratibu.
Miongoni mwa mambo ya msingi ambayo Ujumbe wa Mawaziri na manaibu waziri wakiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Ndugu Nape  Nnauye waliyaongelea na kutaka yachukuliwe hatua za haraka ni pamoja na utunzaji wa mazingira, matatizo ya Ardhi na suala la Kampuni hiyo ya Utafiti wa Madini na Shamba la EFATHA MINISTRY.

ZIARA YA NAPE KATAVI YAZAA MATUNDA, DC AWAFUKUZA WACHINA WALIOKUWA NA MGODI KINYUME NA SHERIA.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe(kulia) akiwa katika eneo la msitu wa Hifadhi ya Katavi, eneo maarufu kwa jina la lyamba ly... [Read More]