Kitua cha Mabasi mjini Moshi kikiwa akina mabasi na abiria wakiwa wamejaa wakisubiri mabasi hayo ambayo madereva wake na wafanyakazi walikuwa wamegoma na kuelekea Ofisi za CCM ili waweze kusaidiwa. |
Na RODRICK MAKUNDI,
MOSHI.
Umati mkubwa wa watu jana ulifurika kwenye ofisi za CCM Moshi mjini wakishinikiza wapatiwe kadi na bendera kwa walichodai kuchoshwa na maamuzi ya CHADEMA yanayowarudisha nyuma kiuchumi.
Watu hao wengi wakiwa wafanyabiashara ya usafirirshaji abiria katika Manispaa ya Moshi, walidai uamuzi huo umetokana na hatua ya CHADEMA kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kupandisha Ushuru wa mabasi ambao unawazidishia ugumu wa maisha na gharama za uendeshaji.
Habari zilisema watu hao wengi wakiwa vijana,m walifika kwenye ofisi za CCM Moshi mjini, saa sita mchana, kwa maandamano ya magari na miguu, kueleza dhamira yao ya kuitosa CHADEMA.
Akizungumzia ujio wa watu hao,Katibu wa Umoja wa Vijana CCM(UVCCM) Moshi, Joel Makwaiya alisema CCM imejitosa kuhakikisha wananchi wanapatiwa ufumbuzi wa kudumu wa tatizo lililojitikeza katika sekta ya usafirishaji na kwamba suala hilo limeanza kushughulikiwa.