Google PlusRSS FeedEmail

MAMA MARIA APOKEA TUZO YA JUU YA HESHIMA ILIYOTOLEWA NA SERIKALI YA BURUNDI KWA BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU JULIUS K. NYERERE.



Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Mama Maria Nyerere, Tuzo ya Juu ya Heshima ya Taifa la Burundi aliyotunukiwa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Burundi yaliyofanyika mjini Bujumbura wiki iliyopita. Mwalimu Nyerere alitunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Burundi ambapo alikuwa mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa nchi hiyo Prince Louis Rwagasore. Rais Kikwete alimkabidhi Mama Maria tuzo hiyo leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Nchi ya Burundi ni moja kati ya nchi ambazo zimeweza kuutambua mchango wa Tanzania na hususani Kwa Hayati Mwalimu Kambarage Nyerere kwa mchango na juhudi kubwa alizoweka kuhakikisha nchi za kiafrika zinajikomboa na kujitawala zenyewe..hayo ni baadhi ya mambo makubwa yaliyofanywa na Kiongozi huyu katika bara letu la Afrika..atabaki kukumbukwa kwa michango yake hiyo.

Leave a Reply