Google PlusRSS FeedEmail

WILAYA YA NACHINGWEA YAGUSWA NA VIFO VYA WATANZANIA AJALI YA BOTI KISIWANI UNGUJA

Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi imemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia Vifo vya Watanzania waliofariki katika ajali ya boti ya Skagit iliyotokea hivi karibuni maeneo ya chumbe kisiwani Unguja.

Salamu hizo zimefikishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Chonjo, ambae alisema kuwa wananchi wake wamemuomba afikishe salamu za rambirambi kwa Mheshimiwa Rais, na ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata majeruhi.

Bi Chonjo alisema kuwa huu ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao ni majonzi yetu, Watanzania wote. Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa.

Aidha  amewapongeza maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa meli binafsi, kwa juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa na maafa haya makubwa na ya aina
yake. Ambapo alisisitiza na kuomba  waendeleze juhudi hizo kwa manufaa ya Nchi yetu.

  ’’Hakika Inauma sana kuona Watanzania wakipoteza maisha  hasa tukikumbuka vifo vingi vya MV Spice Islander miezi 10 iliyopita Wananchi wangu wameniomba nikuombe uunde tume ya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na njia ya kunusuru vifo vya Majini vinavyopoteza nguvu kazi nyingi kwa Maendeleo_Alisema DC. Chonjo" Kutokana na ajali hiyo na msiba huu mkubwa,Tumeungana nawe Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,katika maombolezo ya taifa ya siku tatu.

This entry was posted in

Leave a Reply