Google PlusRSS FeedEmail

Warembo Mjini Kahama wajiunga na CCM.

Wakala wa Miss Tanzania wilaya ya Kahama akiwa na baadhi ya washiriki wa kinyang'anyiro cha kumpata Mrembo wa wilaya ya kahama wakiwa katika Picha ya Pamoja nje ya Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi wilayani humo.


      Katika kuthibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi ni Chama chenye wanachama wa RIKA zote na tabaka zote, tofauti na propaganda za vyama vya upinzani vikiongozwa na Chadema kuwa CCM haina vijana, wanamitindo vijana kutoka wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga waliongozana mpaka ofisi za Wilaya za Chama Cha Mapinduzi na kuchukua kadi zao na wengine kulipia Kadi zao ambazo walikuwa nazo muda mrefu ili kuweza kubaki wanachama hai wa Chama hiko.
Tukio hilo la aina yake liliongozwa kwa shamra shamra na shangwe kwa wananchi wakazi wa wilaya hiyo ya kahama. Mchakato wa kumpata mrembo wa wilaya kutoka wilaya hiyo bado unaendelea ambapo wasichana wapatao 16 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo ya kuiwakilisha wilaya ya kahama katika mashindano ya urembo ya Mkoa.

This entry was posted in

2 Responses so far.

  1. KIYUNGI says:

    Ccm ni chama cha watu wote..

  2. Nawapongeza sana warembo hao kwa uamuzi wao wa busara karibuni CCM chama chenye kutoa matumaini kwa watanzania wa \rika zote...Wao chadomo ndio hawana vijana....CCM in UVCCM ambapo ndipo vuiongozi wote wa nchi hii wamepitia hao jamaa watakua hawana histiria nzuri ya CCM na wala ya serikali yetu.

Leave a Reply