Google PlusRSS FeedEmail

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AKABIDHI VIFAA ZAHANATI YA KIMARA

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi akimkabidhi vifaa vya huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda katika hafla maalum iliyofanyika jana, kwenye Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vya sh. milioni 5.1, vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi wa Jumuia ya Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya Kinondoni, Stanley Mkandawile (wapili kulia), na katikati ya Makamu na Mganga Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk. (Picha na Bashir Nkoromo)
 Baadhi ya wanachama wa Jumuia ya Wazazi waliohudhuria sherehe hiyo.

Wana-CCM na wananchi kwa jumla wakijimwaya mwaya kucheza muziki wa taarab, kushangilia makabidhiano ya vifaa hivyo vya huduma na tiba kwa Zahanati yao.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hiyo ya makabidhiano ya vifaa vya huduma na tiba kwa Zahanati ya Kimara. Kulia (Mwenye koti) ni Diwani wa Kata hiyo ya Kimara kwa tiketi ya Chadema. 

This entry was posted in

Leave a Reply