Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-Itikadi na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo za chama Lumumba ,Dar es salaam. |
YAH; UPOTOSHAJI WA ZIARA ZA CHAMA MIKOANI
Toka tarehe 03/05/2012 nimekuwa na ziara kadhaa za kichama katika mikoa mbalimbali kwa lengo la kukiimarisha Chama. Baadhi ya mikoa niliyofanikiwa kufika ni pamoja na Ruvuma, Njombe, Iringa,Mbeya,Kagera,Rukwa na Katavi. Ziara hizi zimekuwa zikilenga kufanya yafuatayo kati ya mengi niliyofanya:
1. Kukagua uhai wa Chama
2. Kukagua maendeleo ya uchaguzi ndani ya Chama
3. Kukagua miradi mbalimbali ya kiuchumi ya Chama
4. Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM