Tambwe Hiza wa CCM Makao Makuu akihutubia wananchi masuala muhimu ya kujenga nchi na yenye kuleta maendeleo kwa Taifa |
Katibu mkuu wa umoja wa vijana wa CCM Martin Shigela amewataka wananchi wa mkoa wa Mtwara kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao wakati Tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya itakapofika mkoani humo kukusanya maoni ya wananchi,amesema CCM haina agenda yoyote iliyojificha katika upatikanaji wa katiba mpya itakayotokana na utashi wa wananchi wenyewe ,alitilia mkazo kwa wananchi kutoa maoni yao kwa amani bila kuingilia uhuru wa wengine,aliwaasa kuangalia mambo ya muhimu ambayo wanaona yatasaidia kuiweka nchi katika amani na kuendelea kutoa fursa ya maendeleo kwa wananchi kama ilivyo sasa,kuhusu mgombea binafsi alisema CCM haipingi kama wapinzani wanavyotangaza na kama wananchi wanalitaka hilo katika kukuza demokrasia nchini waliseme na litatekelezwa bila wasi wasi na kwamba CCM ndiyo itafaidika zaidi kwa kuwa wanachama wake hawataenda upinzani kutafuta nafasi za kugombea kama ilivyo sasa ambapo wanakwenda huko huku wakiamini vyama hivyo havina sera yoyote ya maendeleo ya Taifa zaidi ya kutaka utawala,alielezea fursa mbali mbali za mkoa huo zilizoletwa na serikali ya CCM na zitakazoendelea kuletwa katika kipindi kifupi kijacho,kabla ya hapo mjumbe aliefuatana naye katika msafara wake Tambwe Hiza alizungumzia hali ya nchi iloivyokwenda mbele kimaendeleo tangu tulipopata uhuru ikiwa nin pamoja na uanzishaji wa shule nyingi za msingi karibu na maeneo wanayoishi wananchi kinyume na hali ilivyokuwa kabla ya kujitawala na miaka ya mwanzo ya uhuru ambapo kila Tarafa ilikuwa na shule moja ya msingi jambo lililopelekea watoto kutembea umbali mkubwa kwenda shule,aliwabeza wanaodai miaka 50 kuwa hakijafanyika kitu kwa kutoa mifano ya ya vyuo vikuu vilivyoanzishwa baada ya uhuru ambavyo havikuwepo kabla idadi ya wanafunzi wanaoingia sekondari hivi sasa akitolea mfano wa idadi ya watoto 5 kati ya watoto 100 waliofaulu waliokuwa wakienda sekondari wakati wa serikali ya awamu ya kwanza kwa kuwa wakoloni hawakujenga za kutosha,wanafunzi waliongezeka kufikia 13 wakati wa awamu ya pili,21 awamu ya tatu na awamu hii ya Rais Kikwete imefikisha 97 kati ya mia huku baadhi ya mikoa ikifikia 100/100