Mdau, kusoma hotuba ya salamu hizo, Tafadhali ingia kwenye ukurasa wa Hotuba, Makala na Maoni binafsi au usiende mbali>> BOFYA HAPA
SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA, TAREHE 31 DESEMBA, 2013
Mdau hizi ni salamu zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu, Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani) katika kuhitimisha mwaka... [Read More]
Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba 31, 2013, vimewasilisha majina ya watu vinaowapendekeza wafikiriwe kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Taarifa iliyotolewa leo mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na kusambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu pia Dar es Salaam, imesema taasisi hizo zimewasilisha majina yao kwa mujibu wa mwaliko uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa makundi yaliyobainishwa katika Kifungu cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83).
Taarifa hiyo imesema kuwa makundi hayo 50 yaliyowasilisha majina yanayopendekezwa kwa ajili ya uteuzi yanatokana na barua 169 zilizopokelewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.
Makundi ambayo yamewasilisha majina ni yafuatayo: Shirika la Wasaidizi wa Jamii Kabila la Wagogo, Tanzania Association of Social Workers (TASOWA), Teachers and Student Forum Tanzania, Tanzania Women Teachers Association, Umoja wa Wanawake Wajane Wilaya ya Karagwe na Kyerwa (UWK), Tanzania Peace and Development Society, Better World Organization (BWO), Youth Focus and Development, Association of Traditional Medicine Man, Registered Centre for Good Governance and Development in Tanzania, Chama Cha Kijamii (CCK), CHANETA na Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania.
Makundi mengine ni Legal Aid Iringa Village, Tanzania Kilolo Orphans and Social Development Organization, Legal aid and Social Welfare Association, Legal and Human Right Centre, Tanzania Lift Initiative NGO, Kilolo Paralegal Unit, Women Development and Social Activities Association, Defence of Human Right/Citizen Rights, DAWSEN Trust Fund, Baruti Development Association (BADEA), Living Hope Ministries Trust, EFATHA Ministry, Bethel Assemblies of God Tanzania, Muslim and Christian Brotherhood Society, Baraza Kuu la Waislamu wa Kondoa – Tanzania na Jesus Temple Inner Transformation News.
Taasisi nyingine ni Jumuiya ya Waithna Asharriyyah Tanzania, Rehmatfi Sabilillah Trust of Tanzania, Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), National Reconstruction Alliance (NRA), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia Makini, African Progressive Part – APPT Maendeleo, National League for Democracy, Tanzania Film Federation, Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni, Al-Amoud General Enterprises, Blue Belt and Water Sources Control, Community Development Training Institute – Tengeru, Tanzania Medical Student Association, Tanzania Sea Farmers Union, Medical Association of Tanzania, Chama cha Wastaafu wa Mbinga, Union of Tanzania Press Clubs, Umoja wa Wanawake Tanzania, Alliance for Tanzania Farmers Party, Tanzania Social Economic and Environment and Wellbeing.
Kwa vile mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo ni tarehe 02 Januari, 2014, Balozi Sefue ametoa mwito kwa makundi mengine ambayo hayajawasilisha orodha hiyo kufanya hivyo kabla muda uliowekwa kuisha. Aidha, wakati wa kuwasilisha ni muhimu kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sheria na kama vilivyofafanuliwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 443 lililochapishwa tarehe 13 Desemba, 2013. Vilevile ni muhimu kuzingatia kuwa majina yanayopendekezwa na Taasisi au makundi yaliyoainishwa kwenye sheria na siyo mtu binafsi kujipendekeza mwenyewe.
Kwa wale watakaojipendekeza wenyewe wajue kuwa watakuwa wanakwenda kinyuma na maelekezo.
KUELEKEA KATIBA MPYA: TASISI ZA KIJAMII, VYAMA VYA SIASA NA VYA KITAALUMA WAPELEKA KWA RAIS WANAOPENDEKEZA WAWEMO BUNGE LA KATIBA
BASHIR NKOROMO, DARES SALAAM Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba ... [Read More]
AMIRIJESHI MKUU, RAIS JAKAYA KIKWETE AMWAPISHA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI TANZANIA LEO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijin... [Read More]
MZEE MWINYI AFUNGUA MAKAO MAKUU YA BPZ MJINI ZANZIBAR
RAIS Mstaaf wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi,akikata Utepe kuashiria kuifunga Makao Makuu ya Benki ya PBZ Ismamic Bank ilioko katika jen... [Read More]
Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Tanzania, Rais Jakaya Kikwete Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imemkariri Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, akisema kuwa Kamishna Mangu (pichani) anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
"Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi", tarifa hiyo imesema.
Taarifa hiyo imesema kuwa pia Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).
Taarifa hiyo imesema, Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
RAIS KIKWETE AMTEUA ERNEST MANGU KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI (IGP), ABDULRAHMAN KANIKI NAIBU IGP
NA BASHIR NKOROMO, DSM Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Tanzania, Rais Jakaya Kikwete Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua K... [Read More]
- Yasema itatafakari na kuamua ipasavyo hoja za Tume
- Yasisitiza mchakato utumike kuwaunganisha Watanzania
CCM YAIPONGEZA TUME YA KATIBA
Yasema itatafakari na kuamua ipasavyo hoja za Tume Yasisitiza mchakato utumike kuwaunganisha Watanzania Chama Cha Mapinduzi kimeipongeza T... [Read More]
Jaji Warioba akikabidhi rasimu hiyo pia kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Rasimu ya Katiba Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya (kushoto) baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Rasimu ya Katiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wastaafu na waasisi wa Tanzania, wakiwa wameshikilia rasimu hiyo, baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana. Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Job Lusinde, Sir George Kahama, Hassan Nassor Moyo na Jaji mstaafu, Mark Bomani na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya
Baadhi ya wananchi na wanazuoni wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa Rais Jakaya Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein, rasimu ya mwisho ya katiba.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba baada ya makabidhiano ya Rasimu ya pili ya Katika katika viwanja vya Karimjee Hall jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia.
Rais Jakaya Kikwete, Dk. Shein, Dk. Bilal, Maalim Seif Sharif Mahad na viongozi wengine wakiwa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
RAIS KIKWETE, DK. SHEIN WAKABIDHIWA RASIMU YA PILI YA KATIBA LEO
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya pili ya Katiba mpya, ... [Read More]
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia akikabidhi msaada wa chakula na vitu mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Tosamaganga Sisita Herena Kihwele. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA |
KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA GNSM CONTRACORS CO. LTD INAYOENDESHA NA GEOFREY MUNGAI YATOA MSAADA WA CHAKULA CHA MWAKA MPYA KWA YATIMA TOSAMAGANGA
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia akikabidhi ms... [Read More]
DIWANI MWINGINE WA CCM AFARIKI DUNIA SHINYANGA
SHUNYANGA, Tanzania Diwani wa CCM katika kata ya Mwakitolyo, katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Kasanga Lumala (75) amefariki dunia... [Read More]
=================
BASHIR NKOROMO, TEMEKE, Tanzania
Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Kibamba, Dar es Salaam, Ayoub Semvua, amesifu kuwa kasi ya utendaji kazi ya mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu ni kubwa na huenda inastahili kwendana na kasi ya utendaji wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itukadi na Uenezi Nape Nnauye.
"Nilipoitwa na rafiki zangu hawa wa Azimio, sikujua kama na wewe utakuwepo, lakini nikawa nimenuia kuwa hata kama hutakuwepo nitakusifia kwa kazi kubwa unayofanya ya kimaendeleo katika kutekeleza ilani ya CCM katika jimbo hili la Temeke... na sasa kuwa nimekukuta nitakusifu hapa hapa, wewe kasi yako ya utekelezaji wa ilani ya CCM inatisha, na kwa kasi hii unaweza kuwa unastahili kasi ya viongozi wetu Ndugu Kinana, Mzee Mangula na Kijana wao Nape", alisema Semvua alipopewa fursa ya kuzungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Azimio, ambacho alikuwa mgeni mwalikwa.
"Huyu Katibu wetu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti Mzee Mangula na kijana wao Nape, kasi yao ni kilometa 140 kwa saa. Kama kuna mtu aliyeingia katika uongozi wa CCM kwa lengo tofauti kasi hii lazima itamshinda na bora ajiondoe mwenyewe mapema", Semvua aliongeza.
Semvua alisema, kutokana na utendaji bora na shirikishi wa Mtemvu, jimbo la Temeke limekuwa na sura tofauti kimaendeleo ikilingtanishwa na miaka 20 ikiongozwa na wabunge mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa sasa wa TLP, Augustine Mtema ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.
"Mfano mzuri wa maendeleo, niliyoshuhudia ambao kila mtu anauona ni barabara za lami zilivyotanda katika maeneo mbalimbali ndani ya Temeke, tangu nimetoka Kibamba nimeteleza kwa lami moja kwa moja bila kugusa udongo hadi naingia kwenye Ofisi hii ya CCM Azimio", alisema Semvua.
Semvua alisema, kutokana na kasi inayoonyeshwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na viongozi wengine kama Mtemvu, CCM itashinda urais ba viti vingi vya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2014.
Aliwataka wana-CCM kuachana na tabia ya kuwa na nongwa aliyoifananisha na ya kinywaji cha kahawa, ambayo baadhi wamekuwa wakidumu nayo kiasi cha kuchagua wapinzani wakidhani wameikomoa CCM kumbe wamejikomoa wenyewe.
"Pale wilaya ya Kinondoni tumepoteza viti viwili vya ubunge na vingi tu vya udiwani na mitaa, sababu kubwa ni nongwa tu. Wanasema, Wakasema aaa, bora tuupe upinzani tuheshimiane. Sasa ukiwauliza pale Kawe na Ubungo kwamba mliwapa ubunge wapinzani sasa heshima gani mnapata? hawana jibu zaidi ya kuinama chini", alisema Semvua.
Akifungua kikao hicho, Mtemvu aliwataka wana-CCM na wananchi kwa jumla kuwapima viongozi kwa utendaji kazi zao na sio kwa uhodari wa porojo nyingi kwa sababu wananchi wanachohitaji ni maendeleo.
Alisema, katika kipindi chake cha Ubunge, Temeke imeweza kuwa na barabara karibu 15 zenye lami hadi pembezoni mwa mji huo na kwamba zile zisizokuwa na lami zimeboreshwa kwa kiwango kibwa kiasi cha kupitika nyakati zote.
SEMVUA: KASI YA MTEMVU INAENDANA NA YA KINANA, NAPE
MWENYEKITI wa CCM Kata ya Kibamba, Ayoub Semvua akimpongeza Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu, baada ya kuzungumza kama mgeni m... [Read More]
![]() |
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowatembelea na kuwafariji baadhi ya wagonjwa katika wodi ya Mwaisela leo.(picha na Freddy Maro). |
RAIS KIKWETE AWAJULIA HALI WAGONJWA WALIOLAZWA MUHIMBILI Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa kat... [Read More]
![]() |
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal baada ya kuwasili. ((Picha na Freddy Maro) |
RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI AKITOKEA MAREKANI KUCHEKIWA AFYA Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete... [Read More]
![]() |
JAJI WARIOBA |
JAJI WARIOBA KUKABIDHI RASIMU KWA RAIS KIKWETE, DK. SHEIN JUMATATU HII
JAJI WARIOBA DAR ES SALAAM, Tanzania Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliuko ya Katiba, Assaa Rashid, imesema, Jumatatu ijayo y... [Read More]
WAJUKUU WAMUUA BABU YAO KWA KIPIGO SIKU YA KRISMAS!!!!
TABOTA, Tanzania Watu wawili wamekamatwa na Polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa tuhuma za mauaji ya babu yao. Watuhumiwa hao ni Mwash... [Read More]
KIONGOZI ADAIWA KUINGIA MITINI TEMEKE, ASAKWA NA WAPIGAKURA WAKE
NA MWANDISHI WETU VIONGOZI wa Jumuia ya Wazazi katika Kata za Temeke, Dar es Salaam, wametoa madai mazito kwa Mjumbe wao wa Baraza Kuu la Ju... [Read More]
Wakizungumza
Rais Kikwete akimshukuru Ki-Moon baada ya mazungumzo yao
Ki-Moon akimvuta pembeni Rais Kikwete kisha..
Akamwambia jambo kabla ya kuagana
RAIS KIKWETE AENDELEA VEMA NA UCHUNGUZI WA AFYA YAKE MAREKANI, AKUTANA NA BAN KI-MOON
Rais Jakaya Kikwete akikaribisha na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moo, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Mare... [Read More]
PINDA APOKEA MSAADA WA PIKIPIKI 44
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama pikipiki mbili kati ya 44 zilizotolewa msaada kwake na Ubalozi wa China nchini pamoja na Kampuni ... [Read More]
WATENGENEZAJI SABA WA MAMBOMU YA KIVITA WASHIKWA KATIKA NYUMBA YA IBADA
Na Oscar Assenga,Korogwe. JESHI la Polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na wakazi wa Kijiji cha Maili kumi wilayani Korogwe wamefanikiwa k... [Read More]