WATU 90 wamekufa na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa vibaya katika shambulio la kigaidi lililotokea leo nchini Yemen.
Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Aljazira, shambulio hilo lililenga wanajeshi nchini humo.
Taarifa zinasema mlipuko huo umetokea baada ya askari mmoja wa Yemen aliyekuwa amesheheni mabomu kujilipua katika eneo la kijeshi.