Na Mwandishi Wetu
Mweneyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete kesho, Jumatatu, May 7, 2012, atawaapisha mawaziri na Manaibu mawaziri aliowateua katika mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri aliyoyatangaza Ijumaa iliyopita Ikulu, Dar es Salaam. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema sherehe za kuaposha mawaziri hao zitafanyika kwenye viwanja vya Ikulu kuanzia saa 5.30 asubuhi.
Ningeshauri Rais aunde Wizara 11, na kuwe na mawaziri wa nchi katika Ofisi ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Nikipewa nafasi ya kutaja wizara hizo nitafanya hivyo
Gerry Paul