Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imejadili kwa kina suala la kupanda kwa gharama za maisha nchini. NEC inakiri kwamba ni kweli lipo tatizo la kupanda kwa gharama za maisha nchini.
Tatizo hili pia limezikumba karibu nchi nyingi za Afrika Mashariki na kwakweli karibu sasa lipo dunia nzima.
Baadhi ya sababu za kupanda kwa gharama za maisha hapa nchini ni pamoja na;
1. Hali mbaya ya mavuno inayotokana na uhaba wa mvua au mvua kunyesha kipindi cha nje ya msimu katika maeneo mengi nchini.
2. Kuongezeka kwa bei ya mafuta duniani, hivyo kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa bidhaa na usafirishaji wa mazao.
3. Kuyumba kwa thamani ya dola ya Marekani.
4. Kuwepo kwa soko huria ambapo sasa mazao ya chakula yanapata soko nje ya nchi, na wakati mwingine kuuzwa nje kwa njia ya magendo na hivyo kusababisha uwepo wa ukubwa wa mahitaji na hivyo kuongezeka kwa bei ya chakula nchini.
5. kuongezeka kwa walaji wakati uzalishaji ukiwa mdogo.
6. kutofanikiwa (ikiwemo kuhujumiwa na wafanyabiashara wasio waaminifu) kwa baadhi ya mikakati ya kudhibiti mfumko wa bei.
Uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa.
1. Pamoja na Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na wa kati za kukabiliana na tatizo hili, CCM inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka za muda mfupi ikiwemo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT katika sukari.
2. Utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea upanuliwe ili kunufaisha wakulima wengi.
3. Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini, hasa kwa kupitia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa, ikiwa ni pamoja na kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula katika maeneo ya uzalishaji wa mazao, na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ununuzi wa mazao hayo. Pamoja na hili, mipango ifanywe kuongeza uwezo wa wakulima kuhifadhi chakula chao wenyewe na kupunguza upotevu baada ya mavuno (post-harvest losses).
3. Serikali iendelee kupanua utaratibu wake wa kutumia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa (SGR) kama nyenzo ya kudhibiti kupanda kwa bei za vyakula. Wakati wa uhaba wa vyakula katika maeneo ya mijini, kasi ya kupeleka chakula maeneo hayo iongezwe na utaratibu mzuri zaidi wa usambazaji wa chakula utumike ili walaji, na sio wasafirishaji na wasindikaji, wanufaike.
4. Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kilimo nchini, hasa ASDP na SAGCOT, ambayo itasaidia kumaliza tatizo la chakula nchini na kuongeza ajira na kipato kwa Watanzania walio wengi.
5. Serikali idhibiti malipo ya huduma ya ndani kwa kutumia fedha za kigeni, hasa dola za kimarekani. Aidha, Serikali iongeze udhibiti wa Maduka na mahoteli yanayofanya biashara ya fedha za kigeni ili kuondoa hujuma kwa uchumi wa nchi inayofanywa kutokana na uhuru uliokithiri katika biashara hii.
6. Waajiri wahimizwe kupandisha mishahara na malipo mengineyo kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha.
7. Serikali iweke jitihada zaidi za kudhibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi za nyumba na usafiri.
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2012
(476)
-
▼
May
(63)
- CCM WILAYA YA KAHAMA WALAANI KAULI ZA MAIGE
- CHADEMA WANAPODANDIA KILA JAMBO KUTAFUTA SIFA!!!!!
- MDAU ANAOMBA MSAADA KWENYE TUTA KUHUSU VIONGOZI WA...
- VICKY KAMATA ATOA MSAADA KWA WALEMAVU, GEITA
- UFAFANUZI KUHUSU TAREHE YA KUCHUKUA NA KUREJESHA F...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA IRAN IKULU
- ZIARA YA MUKAMA MKOA WA PWANI
- UFAFANUZI WA HOTUBA YA UPOTOSHAJI YA MHE. ZITTO KA...
- ASILI YA MFUMO WA SERIKALI MBILI - JULIUS K. NYERERE.
- RAIS JAKAYA KIKWETE AMPOKEA RAIS ALLASANE OUTTARA ...
- CCM YAMTAKA WAZIRI WA KATIBA SMZ AJIUZULU
- DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA FINLAND.
- CHADEMA YAKWAA KISIKI MTWARA.
- ZIARA YA NAPE KUIMARISHA CHAMA BUKOBA
- KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA A...
- MUKAMA ATAKA MAJENGO YALIYOVUNJWA BAGAMOYO YAJENGW...
- RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO BUBUBU,ZANZIBAR HII HAPA
- CCM YAINYONG'ONYESHA CHADEMA WILAYANI MANYONI
- RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI MAHAKAMA YA RUFANI
- 93 WAUAWA NA 300 KUJERUHIWA KWA SHAMBULIO LA KIGAI...
- WAZIRI DK. TEREZYA ATETA NA BALOZI WA BRAZIL NCHINI
- PRESIDENT KIKWETE AT THE G-8 SUMMIT AT CAMP DAVID
- SPIKA MAKINDA APONGEZA UHUSIANO KATI YA TANZANIA N...
- TANZANIA KUWA KATIKA NCHI ZA KWANZA BARANI AFRIKA ...
- TAWI LA OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA...
- NAPE: VYAMA VYA UPINZANI NI VYA HARAKATI TU
- TAWI LA OFISI NDOGO MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA ,D...
- HOJA YA MCHAMBUZI-CHADEMA HAWAJAKOMAA KIDEMOKRASIA.
- PRESIDENT JAKAYA KIKWETE IN WASHINGTON DC
- CCM: MGOMBEA BINAFSI KUWA PIGO KWA VYAMA VYA UPINZANI
- JK: SINA WASI WASI NA UWEZO WA WAJUME WA TUME YA K...
- RAIS KIKWETE AONDOKA DODOMA BAADA YA VIKAO VYA CCM
- TAMKO LA NEC JUU YA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA ...
- TAMKO LA NEC KUHUSU KUKOMESHA TATIZO LA RUSHWA KWE...
- SPIKA ANNA MAKINDA ZIARANI JAPAN
- KATIBU WA CHADEMA ADAIWA KUNG'ATA SIKIO MTU GESTI ...
- HALMASHAURI KUU YA TAIFA ( NEC) IMEUNDA MKOA MAALU...
- JK AZINDUA BLOGU NA TOVUTI RASMI YA CHAMA
- MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA WEB...
- NEC YATEUA MAKATIBU WA WILAYA WA CCM
- KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) CCM CHAF...
- SAFARI YA WAJUMBE WA NEC KWENDA DODOMA LEO
- KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA LEO DODOMA
- RAIS AREJEA NYUMBANI KUTOKA ETHIOPIA
- KATIBU MKUU WA CCM AMJULIA HALI PROF. MWANDOSYA
- KIJANA MWAKIBINGA AWANIA UKATIBU UVCCM KATA YA KAW...
- RAIS KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA HISA LA MITAJI YA M...
- HOJA YANGU NA KAULI YA NASSARI...!
- VICTORIA FOUNDATION, SUSTAINING IMPACT WASAINI MKA...
- BREAKING NEWS! MA-DC WAPYA HADHARANI
- WAZIRI MKUU AMTEMBELEA PROFESA MWANDOSYA
- RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI
- NAPE: CHADEMA WAMEKUBUHU KWA UONGO
- RAIS KIKWETE AWAAPISHA LEO MAWAZIRI WAKE
- MAKALA
- RAIS KIKWETE KUAPISHA MAWAZIRI WAPYA KESHO
- CCM NA FRELIMO KUIMARISHA MAHUSIANO
- GF TRUCKS & EQUIPMENT YAZITAKA HALMASHAURI KUCHANG...
- ZITTO NA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI
- RAIS KIKWETE ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI
- RAIS KIKWETE ATEUA WABUNGE WAPYA WATATU, MBATIA WA...
- MUKAMA AKUTANA NA BALOZI WA NIGERIA.
- HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE KILELE CHA SH...
-
▼
May
(63)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.
hili ni wazo zuri katika kulinda uchumi wetu,kwani hakuna nchi yoyote duniani inaachia uchumi wake kiholela tu,hata hizo nchi zinazojiita kwamba zinafuata uchumi wa soko hazifanyi hivyo hata kidogo,kwa hiyo hili wazo limekuja wakati muafaka kabisa,ila kinachotakiwa wizara husika ya fedha iwe na nia ya dhati kabisa kufanya hivyo na isimuogope mtu yoyote baada ya sheria husika kupewa baraka na mamlaka husika,hongera halmashauri kuu ya chama kwa uamuzi huu.
Mkakati mzuri kabisa pia Nashauri kuhusu Kudhibiti Bei za Vyakula,Maana eneo hili ni Sensitive kwa Maisha ya Wananchi Serikali iandae Utaratibu ambapo ITAUZA MOJA KWA MOJA KWA WANANCHI KWA BEI NAFUU VYAKULA hv badala ya kuwauzia Wafanyabiashara Ambao baadae Huuza Kwa Bei ya Juu na Lawama kurudia Serikali
Ni jambo jema kwa ccm kuendelea kujitathminin na kubaini wapi inaweza kuboresha shughuli zake hasa kwa kuangalia dhima kubwa ya CCM kwamba ndio chama na kimbilio la wanyonge wa Tanzania, Afrika na dunia kwa ujumla wake.
HAWA WAKUU WA WILAYA WAWE CHACHU HASA YA KUTEKELEZA MAADHIMIO YENYE KUWANUFAISHA WATANZANIA, KWELI SASA NI WAKATI MCHANGO WA CHAMA KATIKA JAMII UWE WA KUZUNGUMZIKA NA UNAANZA NA SISI WENYEWE