Tokyo Japan
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (pichani, aliyesimama) amesema, Tanzania inajivunia uhusiano mzuri kati yake na Japan.
Akizungumza katika majumuisho ya ziara yake nchini Japan, Mhe. Makinda amesema, Bunge la Tanzania linaishukuru Serikali ya Japan na Bunge lake kwa kumwalika yeye na Ujumbe wa Wabunge kutoka Tanzania kuja kujifunza maswala Mabalimbali ya Kibunge ikiwa ni pamoja na kukuza demokrasia ya kibunge baina ya nchi hizi Mbili.
Amesema, Pamoja na Japan kupitia katika hali ngumu ya kulipuliwa kwa miji yake miwili ya Hiroshima na Nagasaki wakati wa Vita kuu ya Pili ya Dunia, Matetemeko ya mara kwa mara na mafuriko ya Tsunami, lakaini bado uchumi wake haujayumba kiasi kwamba sasa waJapan wameweza kusima imara kuijenga nchi yao.
Mhe. Makinda amesema Demokrasia safi na Siasa imara za Japan ni mfano tosha na fundisho kwa Tanzania ambapo hivi sasa katika kuimarisha uhusiano huu wa Kibunge, mabunge haya mawili yatabadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa Bunge la Tanzania.
“ Nchini yenu mmekomaa sana katika Demokrasia, ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa shughuli za Kibunge, sisi kama watanzania tuna mengi sana tungependa kujifunza kutoka kwenu, leo mmenialika na ujumbe wangu kutembelea Bunge lenu, lakini napenda kusema huu uwe ndio mwanzo wa kuimarisha uhusiano wetu, ikiwezekana hata kamati zetu za Bunge zipate fursa ya kujifunza kutoka kwenu. Ziara za namna hii zitatusaidia kupanua uelewa wetu katika maswala ya Kibunge“ alisema Mhe. Makinda.
Katika kuhakikisha kuwa Bunge la Tanzania linaimarisha uhusiano wake na Bunge la Japan, Spika Makinda ametoa Mwaliko maalum kwa Spika wa Bunge la Japan Mhe. Takahiro Yokomichi kuja kutembelea Tanzania ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu na wabunge wengine kutoka Bunge la Tanzania.
Mhe. Makinda amesema, Bunge la Tanzania linayo kamati ya Bunge inayoshughulikia maswala ya mambo ya Nje na uhusiano wa Kimataifa, hivyo ni fursa pekee ya kamati hii na wenzao kutoka Bunge la japan kushrikiana kwa karibu kuhakikisha ushirikano huu unakuwa imara na endelevu.
Akimshukuru Mhe. Makinda kwa kukubali mwaliko wake, Spika wa Bunge la Japan Mhe. Takahiro Yokomichi, amesema nchi yake iliichagua Tanzania miongoni mwa nchi za Afrika hususani Africa Mashariki kutembelea Bunge la Japan kwa kuwa ni nchi yenye demokrasia safi na siasa zake zinaimarika kila kukich na kuifanya Japan kuvutiwa na maendeleo hayo katika Bunge la Tanzania.
Mhe. Yokomichi amesema huu ni mwanzo wa ushirikiano muhimu baina ya Mabunge haya mawili ambapo Bunge la Japan pamoja na kuwa na kamati maalum inayoshughulikia maswala ya Afrika, bado kuna haja kwa kamati hiyo kufanya kazi kwa ukaribu na Bunge la Tanzania kwa lengo la kuangalia maeneo muhimu ambayo Japan itaisaidia Tanzania.
Hata hivyo Mhe. Yokomichi ameaidi kuishawishi Serikali yake ya Japan ili iendelee kutenga fungu kubwa zaidi kwa lengo la kusaidia sekta mbalimbali za maendeleo nchini Tanzania. Tarari Japan ni mchangiaji Mkubwa katika sekta mbalimbali za maendelo kwa kiasi kikubwa.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Ujumbe wa wabunge 5 kutoka Bunge la Tanzania upo Japan kwa mwaliko maalum na Bunge la Japan kujadili na kuimarisha ushirikiano baina ya Mabunge haya mawili, ambapo kabla ya kuonana na Mwenyeji wake, Ujumbe huo wa Tanzania ulipata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali ya utalii nchi Japan ikiwa ni pamoja na eneo la Mji wa Natori lililokumbwa na mafuriko yaliotokea machi mwaka jana na Mji wa Hiroshima uliosambaratishwa na Bomu la Atomic wakati wa vita kuu ya dunia mwaka 1945. Spika na Ujumbe wake wanatarajia kurudi nchini jumanne wiki hii.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2012
(476)
-
▼
May
(63)
- CCM WILAYA YA KAHAMA WALAANI KAULI ZA MAIGE
- CHADEMA WANAPODANDIA KILA JAMBO KUTAFUTA SIFA!!!!!
- MDAU ANAOMBA MSAADA KWENYE TUTA KUHUSU VIONGOZI WA...
- VICKY KAMATA ATOA MSAADA KWA WALEMAVU, GEITA
- UFAFANUZI KUHUSU TAREHE YA KUCHUKUA NA KUREJESHA F...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA IRAN IKULU
- ZIARA YA MUKAMA MKOA WA PWANI
- UFAFANUZI WA HOTUBA YA UPOTOSHAJI YA MHE. ZITTO KA...
- ASILI YA MFUMO WA SERIKALI MBILI - JULIUS K. NYERERE.
- RAIS JAKAYA KIKWETE AMPOKEA RAIS ALLASANE OUTTARA ...
- CCM YAMTAKA WAZIRI WA KATIBA SMZ AJIUZULU
- DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA FINLAND.
- CHADEMA YAKWAA KISIKI MTWARA.
- ZIARA YA NAPE KUIMARISHA CHAMA BUKOBA
- KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA A...
- MUKAMA ATAKA MAJENGO YALIYOVUNJWA BAGAMOYO YAJENGW...
- RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO BUBUBU,ZANZIBAR HII HAPA
- CCM YAINYONG'ONYESHA CHADEMA WILAYANI MANYONI
- RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI MAHAKAMA YA RUFANI
- 93 WAUAWA NA 300 KUJERUHIWA KWA SHAMBULIO LA KIGAI...
- WAZIRI DK. TEREZYA ATETA NA BALOZI WA BRAZIL NCHINI
- PRESIDENT KIKWETE AT THE G-8 SUMMIT AT CAMP DAVID
- SPIKA MAKINDA APONGEZA UHUSIANO KATI YA TANZANIA N...
- TANZANIA KUWA KATIKA NCHI ZA KWANZA BARANI AFRIKA ...
- TAWI LA OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA...
- NAPE: VYAMA VYA UPINZANI NI VYA HARAKATI TU
- TAWI LA OFISI NDOGO MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA ,D...
- HOJA YA MCHAMBUZI-CHADEMA HAWAJAKOMAA KIDEMOKRASIA.
- PRESIDENT JAKAYA KIKWETE IN WASHINGTON DC
- CCM: MGOMBEA BINAFSI KUWA PIGO KWA VYAMA VYA UPINZANI
- JK: SINA WASI WASI NA UWEZO WA WAJUME WA TUME YA K...
- RAIS KIKWETE AONDOKA DODOMA BAADA YA VIKAO VYA CCM
- TAMKO LA NEC JUU YA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA ...
- TAMKO LA NEC KUHUSU KUKOMESHA TATIZO LA RUSHWA KWE...
- SPIKA ANNA MAKINDA ZIARANI JAPAN
- KATIBU WA CHADEMA ADAIWA KUNG'ATA SIKIO MTU GESTI ...
- HALMASHAURI KUU YA TAIFA ( NEC) IMEUNDA MKOA MAALU...
- JK AZINDUA BLOGU NA TOVUTI RASMI YA CHAMA
- MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA WEB...
- NEC YATEUA MAKATIBU WA WILAYA WA CCM
- KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) CCM CHAF...
- SAFARI YA WAJUMBE WA NEC KWENDA DODOMA LEO
- KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA LEO DODOMA
- RAIS AREJEA NYUMBANI KUTOKA ETHIOPIA
- KATIBU MKUU WA CCM AMJULIA HALI PROF. MWANDOSYA
- KIJANA MWAKIBINGA AWANIA UKATIBU UVCCM KATA YA KAW...
- RAIS KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA HISA LA MITAJI YA M...
- HOJA YANGU NA KAULI YA NASSARI...!
- VICTORIA FOUNDATION, SUSTAINING IMPACT WASAINI MKA...
- BREAKING NEWS! MA-DC WAPYA HADHARANI
- WAZIRI MKUU AMTEMBELEA PROFESA MWANDOSYA
- RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI
- NAPE: CHADEMA WAMEKUBUHU KWA UONGO
- RAIS KIKWETE AWAAPISHA LEO MAWAZIRI WAKE
- MAKALA
- RAIS KIKWETE KUAPISHA MAWAZIRI WAPYA KESHO
- CCM NA FRELIMO KUIMARISHA MAHUSIANO
- GF TRUCKS & EQUIPMENT YAZITAKA HALMASHAURI KUCHANG...
- ZITTO NA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI
- RAIS KIKWETE ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI
- RAIS KIKWETE ATEUA WABUNGE WAPYA WATATU, MBATIA WA...
- MUKAMA AKUTANA NA BALOZI WA NIGERIA.
- HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE KILELE CHA SH...
-
▼
May
(63)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.