Halmashauri Kuu ya Taifa katika kikao chake kilichofanyika tarehe 13-14 Mei, 2012 mjini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na mambo mengine kilipitisha ratiba ya Chama Cha Mapinduzi ya Mchakato wa kumpata mgombea wa kiti cha Uwakilishi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2012.
Ratiba hiyo imezingatia ratiba ya Tume (ZEC).
1. RATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI YA MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA WA KITI CHA UWAKILISHI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA BUBUBU SEPTEMBA 2012
TAREHE | SHUGHULI |
26-29/7/2012 | Kuchukua na kurejesha fomu ya maombi ya Uongozi wa CCM |
30/7/2012 | Mkutano Mkuu wa Jimbo la Bububu kupendekeza majina matatu (3). |
31/7-4/8/2012 | Kampeni ya Matawini |
5/8/2012 | |
6/8/2012 | Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Magharibi Unguja |
7/8/2012 | Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja |
9/8/2012 | Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa |
11/8/2012 | Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa |
13/8/2012 | Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa |
15/8/2012 | Kamati Kuu ya CCM kufanya uteuzi wa Mgombea |
.
2. RATIBA YA TUME (ZEC) YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUBUBU
TAREHE | SHUGHULI |
22 Agosti -30 Agosti 2012 | Uchukuaji na urejeshaji fomu wagombea |
30 Agosti 2012 | Siku ya uteuzi wa wagombea |
31 Agosti 2012 – 15 Septemba 2012 | Kampeni za wagombea |
16 Septemba 2012 | Siku ya kupiga kura |
.
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
22/05/2012