Google PlusRSS FeedEmail

CCM NA FRELIMO KUIMARISHA MAHUSIANO


ZANZIBAR
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuwa uhusiano  wake na Chama cha Frelimo cha Msumbiji utadumishwa milele ili kulinda maslahi ya vizazi vya nchi hizo.
 
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi ndugu Issa Haji Ussi Gavu ameyasema  hayo leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, wakati akizungumza na Ujumbe wa watu watano kutoka Chama cha FRELIMO, uliongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya FRELIMO Bibi Couccita Sortane.
 
Amesema kimsingi CCM ambacho ni mrithi wa vyama vya ASP na TANU , kati yake na  FRELIMO vina historia na mahusiano yaliodumu kwa miaka mingi, hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha kuwa hazina hiyo inalindwa kwa nguvu zote kwa maslahi ya Tanzania, Zanzibar na Msumbiji.
 
Amesema vyama vya ASP, FRELIMO na TANU vilikabiliwa na vizingiti hatari vilivyowekwa kwa hila za wakoloni, lakini kutokana na juhudi na dhamira zake kuwa njema, hatimae viliweza kuikata minyororo ya kutawaliwa.
 
Gavu amesema wananchi wa Tanganyika walianza kufurahia matunda ya Uhuru wao mwaka 1961, Zanzibar ikafanya Mapinduzi matukufu mwaka 1964 na FRELIMO ikaudondosha Utawala wa Wareno mwaka 1975.
 
Naye Bibi Sortane, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya FRELIMO amesema Chama chake kitaendelea kuthamini juhudi na mchango mkubwa wa hali na mali uliotolewa na vyama vya ukombozi vikiongzwa na Chama Cha Mapinduzi na kuifanya Msumbiji na wananchi wake kuwa huru na kujitawala.
 
Bibi Sortane amesema ni jukumu la vyama vya CCM na FRELIMO kuhalkikisha wanakabiliana na tishio lolote la maadui wa ndani na nje wenye lengo la kuirudisha tena Afrika katika kiza cha Ukoloni Mamboleo.
 
Aidha, Ujumbe huo wa FRELIMO umetembelea sehemu mbali mbali za kihistoria ikiwa ni pamoja na kuzuru kaburi la Mwasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Kwanza wa ASP na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume.
 
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
 
Sgd.
IMETOLEWA NA :-
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI - CCM,
ZANZIBAR.

This entry was posted in

Leave a Reply