Google PlusRSS FeedEmail

CHADEMA YAKWAA KISIKI MTWARA.

Chadema imekiri hadharani kuwa Mkoa wa Mtwara ni ngome imara ya CCM isiyoyumba, anaripoti Chris Mauma kutoka Mtwara.
     Chadema kimekiri hivyo mbele ya kadamnasi ya watu katika mkutano wake uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara.
      Katika mkutano huo tofauti na matarajio ya Chadema kuwa watapokea wanachama wengi kutoka  CCM hadi mkutano huo unamalizika saa 12 jioni, hakuna hata mmoja aliehamia licha ya viongozi wa Chadema kujitahidi kuwashawishi kwa maneno kadhaa wa kadhaa ya ghiliba jukwaani.
      “Wale wanachama wa CCM wanaohamia Chadema njooni  jukwaani kukabidhi kadi za CCM”  aliita Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe  mara kadhaa na kuambulia patupu katika mkutano huo.
       Kama ilivyokuwa katika hotuba za viongozi wenzake waliyomtangulia kuhutubia katika mkutano huo Mbowe aliwashambulia wananchi wa mkoa wa Mtwara kwa msimamo wao usiyoyumba wa kuwa na imani na CCM na kudai kuwa ndiyo sababu iliyowafanya kutokushughulika na mikoa hii katika kueneza
Chama Chao.
     ”Mtwara mnafanya mchezo na mustakabali wa ukombozi wa taifa” alisema Mbowe baada ya kuona hotuba zilizotolewa za  maneno ya kila aina ya ghiliba na uchonganishi kwa wananchi dhidi ya CCM na serikali yake hayazingatiwi.
      “Haya maneno yaliyosemwa hapa na viongozi wenzangu walionitangulia ingekuwa mikoa mingine watu wangekuwa wanalia lakini hapa ninyi mnacheka tu!” alisema Mbowe.
       Katika suala la Urais Mwenyekiti huyo alidokeza kwa kueleza kuwa  katika Chama Chake hakuna alie maalum na haki ya kipekee kugombea, mtu yoyote anaweza kama atakidhi sifa zinazotakiwa bila kujali nafasi yake ya uongozi katika Chama.
   Kama Mbowe,  mapema Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilboad Slaa naye alionyesha kusikitishwa
na msimamo wa  wananchi wa mikoa hii baada ya kuja kueneza Chama miaka kumi iliyopita kijiji hadi kijiji lakini hawakuambulia mafanikio yoyote ya kuimarika na badala yake CCM iliendelea kuwa imara.
      “Kuna watu wanadai kuwa Chadema imeitenga mikoa ya Mtwara na Lindi,hapana hao wanaosema hivyo wamesahau historia ya Chama Chetu” Alisema Dr Slaa.
      Alifafanua kuwa mwaka 2004 walitembelea mkoa mzima huu kijiji hadi kijiji na kuibua shida kubwa ya maji huko vijijini iliyompelekea waziri wa maji wa wakati huo Edward Lowasa kuja kushughulikia tatizo
hilo.
      Lakini baada ya ziara hiyo chama kiliendelea kudodora katika mikao hii ambapo wao waliamua kuiachia CUF ambao kwa kiasi walikuwa wakiambulia wanachama katika wilaya za pwani pwani kama Kilwa na Lindi mjini.
      Wengi waliohudhuria mkutano huo walikuwa ni wanachuo wa Chuo kikuu cha Stella Maris  ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo waliokuwa wakishangilia wahutubiaji.
     “Unajua pale wanafunzi ndio waliokuwa wengi sana na watu kutoka maofisini, wananchi wa kawaida  walikuwa wachache sana, hii inamaana huko mawilayani wanakokwenda ambako wanachuo hawapo watapata shida sana hawatapata watu” alisema mwananchi mmoja.
        Chadema watakuwa katika mikoa hii ya Mtwara na Lindi kwa siku 14 wakijigamba kufanya kama walivyofanya mwanzo kwenda kijiji hadi kijiji, na walijigawanya katika kata mbali mbali za mjini Mtwara.

This entry was posted in

9 Responses so far.

  1. Unknown says:

    Hawa Chadema wanadhani watawadanganya wananchi wote kwa propaganda zao! Safi sana wananchi wa Mtwara!

  2. Unknown says:

    Hawa Chadema wanadhani watawadanganya wananchi wote kwa propaganda zao! Safi sana wananchi wa Mtwara!

  3. bora wakose kabisa kwani wamekuwa wakieneza uchochezi tu na siasa za majukwaa.wawaachie CCM tu cdm bado sna kuongoza nchi.Shibuda analijua hilo wakiwa na Zitto Kabwe

  4. unaweza kuweka picha mbili tatu tuone hali halisi ilivyokuwa?

  5. KIYUNGI says:

    At least after 20 years ndo chama kinaweza kuzungumzia kuongoza nchi kwani angalau kitakuwa na hazina ya kutosha ya viongozi.

  6. Venny says:

    Nilikuwepo pale, hali ilikuwa tofauti

  7. Safi sana wana Mtwara wana CCM wenzangu tusikubari kudaganjwa na Chadema hao ni wanafiki kwani yakwao awayasemi kama Nassari aliyoyasema Arusha ingekuwa CCM ndio wamesema ndio ingekuwa ajenda ya kuu kama kweli ukitaka kujua kuwa wababaishaji angalia majimbo yalio nyakuliwa na chadema hakuna lolote walilolifanya

  8. wadau sio lindi na mtwara tu kifupi wananchi tumeshawastukia wataendelea kupoteza UMAARUFU kwa kuwa agenda zao ni NYEPESINYEPESI si za kudumu unaweza kufananisha na BAZOKA/JOJO/BIG G zina msisimko wa kitambo baada ya muda KWISHA

  9. Hizo ni propaganda za CCM!! CCM imekaliwa kooni. Jiandaeni kung'oka madarakani

Leave a Reply