Google PlusRSS FeedEmail

KATIBU WA CHADEMA ADAIWA KUNG'ATA SIKIO MTU GESTI JIJINI MWANZA

Katibu wa Chadema wa wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, Abel Mwesa,  anatuhumiwa kumng’ata sikio kijana mmoja wa Mtaa wa Nyambiti, baada ya kunyimwa chumba cha kulala na mpenzi wake, wakati wakitaka kufanya mapenzi.

Mwesa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtaa huo, anadaiwa kumng’ata sikio Razaro Norbert (25) Aprili 26 mwaka huu saa 5 usiku, katika Nyumba ya kulala Wageni ijulikanayo kwa jina la Amani, mtaani Nyambiti

Pamojaa na tukio hilo kuripotiwa kituo cha polisi cha Nyakato, mtuhumiwa huyo ambaye anadaiwa kujiita Rais wa Mtaa wa Nyambiti, hajakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria na hivyo kumfanya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, aagize Mwesa akamatwe mara moja.

Akisimulia mkasa huo jana ofisini kwa Mkuu wa mkoa, Norbert alidai kwamba, siku ya tukio mkasa ulianza baada ya kukataa kumpa Mwesa chumba cha kulala wakati akiwa na mwanamke mmoja aliyedai ni mpenzi wake.

“Nilimwambia mimi siyo mhudumu wa Gesti hiyo hapo, nafanya biashara ndogondogo tu, akachukia sana na kuanza kufoka kuwa yeye ndiye Rais wa Mtaa huo ntamnyimaje chumba, ndipo akapiga simu kwa 'makamanda' wake wawili wakaja kunikamata na kuanza kunipa kipigo.” Alieleza.

Alizidi kudai kwamba, wakati wakimshushia kipigo, ndipo Mwenyekiti wake alipomshika kwa hasira na kumng’ata sikio la kulia na kuliondoa lote ambalo sasa linavuja usaha baada ya kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Kijana huyo alidai kwamba, pamoja na kuripoti katika kituo cha polisi cha Mwatex siku hiyo (NY/RB/3059/2012) na kupatiwa PF3 kwa ajili ya matibabu, hadi jana akilalamika kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, mtuhumiwa alikuwa hajakamatwa huku askari wa kituo hicho wakizidi kumsshinikiza apewe fidia ya shilingi 200,000/= na kuachana na kesi hiyo.

Kijana huyom pia alidai kuwa toka wakati huo amekuwa akipewa vitisho vya kuuawa kwa maneno na kuandikiwa barua ambayo imechorwa kaburi (tunayo) ambayo alionyesha kwa Mkuu wa mkoa.

Akitoa agizo lam kukamatwa kwa Mwesa ambaye pia ni Katibu wa Chadema wa wilaya ya Ilemela, Mhandisi Ndikilo alisema “Kituo cha Mwatex kinamaslahi na Mwesa ambaye anadaiwa kujiita Rais wa Mtaa huo anaweza kumaru hata maduka yafungwe.”

This entry was posted in

Leave a Reply