Google PlusRSS FeedEmail

HALMASHAURI KUU YA TAIFA ( NEC) IMEUNDA MKOA MAALUM WA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NA KUCHAGUA MAKATIBU WA MIKOA (9)

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikweete
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeunda Mkoa Maalum wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kufanya uteuzi wa makatibu tisa wa mikoa. 
Taarifa iliyotolewa leo mjini Dodoma, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi Nape Nnauye imewataja Makatibu walioteuiwa na mikoa yao kwenye mabano kuwa ni wafuatao;-

1.     Ndg. Elikana Mauma               (Mkoa wa Mara)
2.     Ndg. Hilda Kapaya                  (Mkoa wa Geita)
3.     Ndg. Shaibu Akwilombe         (Mkoa wa Simiyu)
4.     Ndg. Hosea Mpagike               (Mkoa wa Njombe)
5.     Ndg. Alphonce Kinamhala     (Mkoa wa Katavi)
6.     Ndg. Aziza R. Mapuri              (Mkoa wa Magharibi)
7.     Ndg. Maganga Sengerema    (Atapangiwa kituo)
8.     Ndg. Adelina Geffi                    (Atapangiwa kituo)
9.     Ndg. Christopher Ngubiagai  (Mkoa Maalum wa Wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu)
           
Kuundwa kwa mkoa maalum wa wanafunzi wa elimu ya juu kunalenga kupanua wigo ikiwa ni mkakati wa chama kujiimarisha zaidi kwa wanachama wake wa kada mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa elimu ya juu.
 Uamuzi huu utawapa fursa wanafunzi wasomi ambao wengi wao ni vijana kupata fursa za kikatiba na kanuni kushauri na kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya ngazi ya juu katika chama cha Mapinduzi (CCM).

This entry was posted in

2 Responses so far.

  1. that is good idea ,simply because educated figures especially youths,have lost hope totally,that can make good communication channel,inorder to understand their contribution towards national developments.
    Rgds
    Paul mahondo
    ccm party member.

  2. Mani says:

    WHAT ABOUT SPECIAL REGION OF YOUNG GENERATION OF WORKERS?

Leave a Reply