Kumb. Na. CMM/C/T.10/3/2/VOL.V/47 Tarehe: 31/5/2012
Makatibu wa Mikoa,
Chama Cha Mapinduzi,
TANZANIA.
UFAFANUZI KUHUSU TAREHE YA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU KWA NAFASI ZOTE AMBAZO UTEUZI WAKE WA MWISHO HUFANYWA NA HALMASHAURI
KUU YA TAIFA
Tafadhali rejeeni barua Kumb. Na. CMM/C/T.10/3/2/VOL.V/46 ya tarehe 23/5/2012 yahusika na kichwa cha habari hapo juu.
Mnajulishwa kuwa tarehe ya kuchukua na kurejesha Fomu kwa nafasi zote za CCM na Jumuiya ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa ambazo
uteuzi wake wa mwisho hufanywa na Halmashauri Kuu ya Taifa ni kuanzia tarehe 1/8/2012 hadi tarehe 6/8/2012 badala ya tarehe 2/6/2012 hadi 10/6/2012.
Uamuzi huo ni baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya tarehe 14/5/2012 kuzingatia kuwa muda ni mrefu mno kati ya tarehe za kuchukua/kurejesha fomu na tarehe za mchakato wa kujadili Wagombea hao ambao unaanza tarehe 7/9/2012.
Nawasilisha kwa hatua za utekelezaji.
KIDUMU CHA MAPINDUZI
Francis K. Mwonga
KATIBU WA SEKRETARIETI YA
HALMASHAURI KUU YA TAIFA