Google PlusRSS FeedEmail

KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA LEO DODOMA

Nape
Kamati Kuu ya CCM, inakutana leo mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete na baadaye kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kitakachofanyika kesho.

Katika vikao hivyo CCM itajadili mambo mbalimbali ikiwemo ughali wa bei za vyakula na kero mbalimbali zinazogusa wananchi.

"Kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakilalamika hali ngumu ya maisha na kupanda kwa bei ya vyakula, hivyo NEC itapata taarifa ya serikali kuona hali ikoje na kuangalia nini kifanyike kupunguza au kuondokana kabisa na hali hiyo", alisema Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi kuuambia kwa simu mtandao huu.

Nape alisema ajenda nyingine katika kikao cha NEC ni mchakato wa katiba mpya akisema ni lazima chama nacho kijadili ili kuona mapendekezo na mawazo ya Chama kuhusu mchakato huo.

Alisema pia CCM inatarajia kujaza nafasi zilizo wazi za makatibu wa mikoa na wilaya kwa kuwa kuna maeneo yamebaki wazi kutokana na watendaji wake kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya katika uteuzi uliofanywa hivi majuzi na Rais Kikwete.

This entry was posted in

2 Responses so far.

  1. vyakula vimepanda sana bei. mfano mchele ulikuwa Tsh. 600 mwaka 2005, ukawa Tsh. 1500 mwaka 2010 sasa ni Tsh. 2900 tunatarajia utakuwa Tsh. 5000 ifikapo 2015.

Leave a Reply