WANACHAMA 3,600 kutoka vyama mbalimbali vya Upinzani kikiwemo CHADEMA, wameomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mbeya Mjini.
Miongoni mwao, wapo zaidi ya vijana 200, wanaojishughulisha na kazi na ushonaji magari katika eneo la Forest.
Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya mjini Mwalimu Mwangwala, aliyasema hayo alipokuwa akizungumzia mikakati ya Chama katika kujipanga upya ili kukabiliana na vyama vya upinzani mjini hapa.
Mwangwala alisema “Kabla wanachama hawa hawajajiunga rasmi na CCM, ni lazima wapewe mafunzo kwanza, hatutaki kuwapa kadi za papo kwa hapo kama wafanyavyo CHADEMA au vyama vingine, nia ni kuepuka kuingiza mamluki ndani ya Chama.”
Kwa Habari zaidi soma Gazeti la UHURU leo