Dr. Fenela Mukangara apata ajali ya gari maeneo ya Nzega.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Dr. Fenella Mukangara amepata ajali ya Gari maeneo ya Nzega mkoani Tabora, akiwa njiani akielekea jijini Mwanza ambako alialikwa kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya Taifa ua mchezo wa vishale maarufu kama (DARTS) ambapo katika ajali hiyo watu wote walitoka salama ila baadhi walipata majeraha madogo madogo.