Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Balozi wa Canada nchini Mhe. Robert J. Orr |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Asubuhi ya leo, tarehe 06 Juni 2012, alimkaribisha Balozi wa Canada nchini Tanzania, ambaye amemaliza muda wake Mhe. Robert J. Orr. katika Ofisi yake iiliyopo maeneo ya Ikulu Jijini Dar es salaam.
Balozi huyo alimtembelea Makamu wa Rais kwa lengo la kufanya nae mazungumzo ya kuagana, kwa kuwa muda wa Balozi huyo kuwepo nchini umekwisha. Akizungumza na Makamu wa Rais, Balozi Orr aliendelea kusisitiza kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi yake ya Canada utaendelea kuimarika licha ya kuwa yeye kuondoka Tanzania.
Makamu wa Rais. Dkt Mohammed Gharib Bilal akiagana na Balozi Robert. J Orr. |