Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti aina ya Mroliondo katika eneo la Chem chem ya Maji Njoro,leo Juni 03, 2012, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
Kwa muda mrefu sasa, Makamu wa Rais amekuwa mwanamazingira aliye mstari wa mbele katika usimamizi na uboreshaji wa mazingira na hali ya hewa kwa ujumla. Amekuwa akishiriki katika ziara mbalimbali za kimazingira na hali ya hewa ndani na nje ya nchi.