Google PlusRSS FeedEmail

MUKAMA: CHADEMA IGENI TABIA YA BOB MAKANI KATIKA UONGOZI WA SIASA

NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amewataka viongozi wa CHADEMA kufuata maadili, sifa na hekima alizokuwa nazo muasisi wa chama hicho, marehemu Bob Makani, katika uongozi wa kisiasa.
       Amesema, Makani alikuwa mwanasiasa asiye na maneno mengi majukwaani lakini mweledi wa uongozi ambaye alikwepa kuwatenganisha watu, kisiasa, kidini na kikanda.
      Mukama aliyasema hayo leo katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Makani, kwenye viwanja vya Karimjee mjini Dar es Salaam, sherehe zilizoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.
     Alisema umahiri wa marehemu huyo ulimuwezesha kushika nafasi mbalimbali za juu za uongozi katika utumishi wa umma, ikiwemo Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa kwanza Chadema.
    "Nyadhifa alizokuwa akishika marehemu, haikuwa bahati mbaya, ni kutokana na uelewa na umakini mkubwa aliokuwa nao, aliweza kuwa hata Katibu Mkuu wa CHADEMA, akiwa ni miongoni mwa watu tisa walionazisha chama hicho, lakini akiwa ndiye pekee kutoka eneo walikotoka wenzake hao," alisema.
      Akitoa salamu za vyama vya upinzani, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema marehemu Makani alikuwa si mmbaguzi na alikuwa muadilifu, hivyo aliwataka viongozi wa CHADEMA kuiga mfano wake.
       Alisema heki na busara alizokuwa nazo marehemu huyo zilimuwezesha kushika nyazifa mbalimbali za uongozi serikalini na hata ndani ya Chama chake.
        Kwa upande wake, Rais Kikwete, alisema marehemu Makani atakumbukwa kwa mambo mengi aliyoifanyia nchi akiwa mtumishi wa umma na kwamba alikuwa muadilifu na aliyekuwa akishirikiana na viongozi wengine. HABARI HII KWA KINA  SOMA UHURU KESHO

This entry was posted in

One Response so far.

  1. KIYUNGI says:

    Jamani ccm acheni mambo ya kizamani,hili gazeti la uhuru anzisheni website yenu mwende na wakati.

Leave a Reply