Miongoni mwa Nembo muhimu za Taifa letu ni pamoja na Mwenge wetu wa Uhuru, ambao hubeba falsafa ya kumulika ukombozi na kujaza maarifa watanzania. Ni miongoni mwa vitu vyenye kuwajenga na kuwaongezea Watanzania Ari ya kujiletea maendeleo. Mwenge Huu huwashwa kila Mwaka na kutembezwa Nchi nzima kupita katika kila mkoa, wilaya, kijiji na kitongoji.
Tangu kupatikana kwa Uhuru, Mwenge ulikuwa ukitumika kuhimiza uzalendo, uwajibikaji na kueneza ujumbe mbalimbali ambao unahusu maisha ya Mtanzania, kama vile kupinga Rushwa na Athari zake, Kupigana na Ufisadi na Ubinafsi, Kuhimiza Elimu na Afya na mengineyo. Hivyo mwenge wa Uhuru umekuwa ni Nembo muhimu katika kuikuza Tanzania kama Taifa huru linalojitegemea.
Mbio hizi za mwenge kwa sasa ziko Mkoani Lindi, ambapo Kiongozi huyo wa mwenge amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kisima cha Maji katika Shule ya Msingi Mkupama.
Miongoni mwa Miradi ya Maendeleo iliyozinduliwa Mkoani Lindi, jana na Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru. |