|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais wa Somalia, Sheikh Shariff Ahmed.
|
|
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Rais wa Somalia, Sheikh Shariff Ahmed jijini Arusha, leo june 2, 2012 na kufanya mazungumzo na Rais huyo wa Somalia juu ya mambo mbalimbali yanayoikabili nchi hiyo kwa sasa.
Pamoja na mambo mengine Rais Kikwete na mgeni wake waliongelea juu ya hali ya usalama katika nchi ya Somalia iliyopo katika eneo muhimu la pembe ya Afrika. Nchi ya Somalia kwa muda mrefu sasa imekuwa katika hali tete kiusalama ambapo vikundi mbalimbali vya kikabila vikiongozwa na kikundi cha kigaidi cha al shabab vimekuwa vikifanya mashambulizi ya mara kwa mara kwa raia na viongozi wa Serikali ya Somalia.
Rais Kikwete, alimhakikishia Sheikh Shariff kuwa atampa ushirikiano wa kila aina katika kuhakikisha utulivu na amani vinarejea nchini Somalia.
Rais Kikwete yupo jijini Arusha ambako amefungua na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaoendela katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha.
|
Rais Kikwete akiongozana na ujumbe uliofuatana na Rais, Sheikh Shariff Ahmed wa Somalia. |