Google PlusRSS FeedEmail

VIJANA WA KILAKALA WAUNGANA KUFANYA KAZI YA SANAA KUELIMISHA UMMA

Vijana Kutoka Yombo,Kilakala Wilaya ya Temeke wameungana pamoja na kufanya kundi linalofahamika kwa jina la NEW MSIMAMO, Vijana hao wakiwa chini ya uongozi wa Bw.Said Rashid Kihunda,wameainisha sanaa za aina nne wazofanya, ikiwemo sanaa ya maigizo ya luninga,maigizo ya jukwaa,sanaa ya kucheza ngoma na sanaa ya uimbaji.
  New Msimamo imejikita upya kwenye shughuli za sanaa baada ya kundi la awali la Msimamo la mwaka 2007 kupagaranyika.
  Moja ya Malengo makubwa ni kukusanya vijana pamoja, kuelimisha umma haswa kujiepusha na madawa ya kulevya na magonjwa ya hatari kama ukimwi na mengineyo.
  Kundi hili pia limeamua kujikita zaidi katika uchezaji wa sinema,ingawa mpaka sasa hawajapata ufadhili wa uhakika.


Wasanii wa kundi la New Msimamo wakiwa kwenye picha ya Pamoja baada ya mazoezi.
   Kundi hili linapatikana kwa shughuli zote za kisanaa na kijamii pia unaweza wasiliana nao kwa namba zifuatazo 0652496046/0654999511.

This entry was posted in

Leave a Reply