NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amewataka viongozi wa CHADEMA kufuata maadili, sifa na hekima alizokuwa nazo muasisi wa chama hicho, marehemu Bob Makani, katika uongozi wa kisiasa.
Amesema, Makani alikuwa mwanasiasa asiye na maneno mengi majukwaani lakini mweledi wa uongozi ambaye alikwepa kuwatenganisha watu, kisiasa, kidini na kikanda.
Mukama aliyasema hayo leo katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Makani, kwenye viwanja vya Karimjee mjini Dar es Salaam, sherehe zilizoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema umahiri wa marehemu huyo ulimuwezesha kushika nafasi mbalimbali za juu za uongozi katika utumishi wa umma, ikiwemo Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa kwanza Chadema.
"Nyadhifa alizokuwa akishika marehemu, haikuwa bahati mbaya, ni kutokana na uelewa na umakini mkubwa aliokuwa nao, aliweza kuwa hata Katibu Mkuu wa CHADEMA, akiwa ni miongoni mwa watu tisa walionazisha chama hicho, lakini akiwa ndiye pekee kutoka eneo walikotoka wenzake hao," alisema.
Akitoa salamu za vyama vya upinzani, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema marehemu Makani alikuwa si mmbaguzi na alikuwa muadilifu, hivyo aliwataka viongozi wa CHADEMA kuiga mfano wake.
Alisema heki na busara alizokuwa nazo marehemu huyo zilimuwezesha kushika nyazifa mbalimbali za uongozi serikalini na hata ndani ya Chama chake.
Kwa upande wake, Rais Kikwete, alisema marehemu Makani atakumbukwa kwa mambo mengi aliyoifanyia nchi akiwa mtumishi wa umma na kwamba alikuwa muadilifu na aliyekuwa akishirikiana na viongozi wengine. HABARI HII KWA KINA SOMA UHURU KESHO
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2012
(476)
-
▼
June
(73)
- MAONYESHO YA BUSINESS DEVELOPMENT GATEAWAY YAHITIM...
- Mbunge wa Korogwe Vijijini Prof. Maji Marefu aomba...
- Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Stephen Wassira ...
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya...
- Dr. Fenela Mukangara apata ajali ya gari maeneo ya...
- DR. ASHAROSE MIGIRO AAGWA RASMI UMOJA WA MATAIFA (UN)
- Mkurugenzi wa PharmAccess International ahudhuria ...
- Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba...
- CCM YAFUNIKA MOROGORO SIKU YA JUMAMOSI KATIKA MAHA...
- NAPE ANOGESHA MAHAFALI YA WANA-CCM CHUO KIKUU CHA ...
- MAWAZIRI WA MAZINGIRA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WA...
- RAIS KIKWETE AMPOKEA RAIS WA JAMHURI YA KIARABU YA...
- Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Ash...
- MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU AWAPA DARASA WANAFUNZ...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KAT...
- MH. DKT JAKAYA M. KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUN...
- BUNGENI LEO DODOMA
- VIJANA WA KILAKALA WAUNGANA KUFANYA KAZI YA SANAA ...
- WATUMISHI WA UMMA KUKOPESHWA NYUMBA
- RAIS KIKWETE ATEMBELEA SHAMBA LA MFANO KIJIJI CHA ...
- SBL YAZINDUA MRADI WA UVUNAJI MAJI YA MVUA IRINGA
- ZIARA YA KATIBU WA NEC, ASHA ABDALLAH JUMA MKOANI ...
- MWANDISHI WILLY EDWARD OGUNDE AAGWA LEO
- MYIKA ALIPORTIMULIWA BUNGENI
- RAIS KIKWETE AAPISHA MWENYEKITI MPYA NA MAKAMISHNA...
- HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATI...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWANA WA MFALME NA NAIBU W...
- RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEWAAPISHA WAJUMBE SIT...
- RAIS KIKWETE ATUMA SALAAM ZA RAMBI RAMBI ,KUOMBELE...
- CCM YAFUNIKA IRINGA MJINI
- ZIARA YA NAPE KILOLO MKOANI IRINGA
- TAARIFA MAALUM KUTOKA TAWI LA CCM-WASHINGTON.
- MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA ...
- NAPE AKUTANA NA WALIMU WA SEKONDARI NA MSINGI MAFI...
- NAPE ATAKA WAKATAJI MBAO WADOGO MAFINGA NAO WAPEWE...
- NAPE AKAGUA CHUO CHA CCM, IHEMI MKOANI IRINGA LEO ...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MRADI WA KUINUA ...
- CCM IPO IMARA SANA MUFINDI MKOANI IRINGA
- WAZIRI WA FEDHA AWASILISHA BAJETI 2012-2013 BUNG...
- RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA BARAZ...
- SHINA LA WAJASIRIAMALI WA CCM STENDI YA MABASI MJI...
- MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM S...
- KATIBU MKUU WA CCM, AKABIDHI TREKTA KWA WAKULIMA W...
- SAITOTI KUZIKWA JUMAMOSI
- RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AMWAPISHA RAS WA MKOA W...
- KITABU KIPYA CHA FASIHI CHAKABIDHIWA KWA MHESHIMIW...
- CCM yavuna wanachama 3,600 upinzani
- MUKAMA: CHADEMA IGENI TABIA YA BOB MAKANI KATIKA U...
- RAIS KIKWETE AONGOZA KUAGWA MWILI WA BOB MAKANI
- NAPE, GUNINITA WAMJULIA HALI JOSEPH SELASINI WA CH...
- CHADEMA YAPASUKA
- Mgombea Urais Kenya afariki ajalini........
- MWENGE WA UHURU MKOANI LINDI.
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA KWA...
- KATIBU MKUU WA CCM, Ndg W. MUKAMA AHUDHURIA MKUTAN...
- LIVE: KUTOKA JANGWANI:
- TANGAZO LA MKUTANO WA HADHARA WA CHAMA CHA MAPIND...
- MWENEZI WA TAIFA-CCM NDANI YA NJOMBE.
- RAIS KIKWETE ACHANGISHA BILIONI 3.2 KATIKA HARAMBE...
- NAPE:ARDHI IKIMILIKIWA NA WATU BINAFSI WANYONGE WA...
- MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGANA NA BALOZI WA CANAD...
- SEMINA ELEKEZI YA MAKATIBU WA CCM WILAYA.
- NAPE AIPONDA OPERESHENI 'VUA GAMBA VAA GWANDA' YA ...
- MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA WABUNGE WA TANZANIA KATIKA...
- SERIKALI YA FINLAND KUSAIDIA MPANGO WA MATUMIZI BO...
- ZIARA YA NAPE SONGEA, HAIJAPATA KUTOKEA...!
- MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA SI...
- MKUTANO WA BARAZA LA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA SOMALIA.
- VIJANA ELIMU YA JUU IRINGA, WAFAGILIA MAGEUZI NDAN...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI MK...
- NAPE AKAGUA MAENDELEO UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAN...
-
▼
June
(73)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.
Jamani ccm acheni mambo ya kizamani,hili gazeti la uhuru anzisheni website yenu mwende na wakati.